Abby Chams Aingia Kwenye Ramani ya Dunia Kupitia Rolling Stone

Abby Chams Aingia Kwenye Ramani ya Dunia Kupitia Rolling Stone

Mwanamuziki chipukizi mwenye kipaji cha kipekee, Abigail Chams maarufu kama Abby Chams, ameweka historia mpya kwa kuonekana kwenye Jalada (Cover) ya toleo la Mei la jarida maarufu la Rolling Stone Africa. Katika toleo hilo, Abby ametajwa kama “Future of Music”, ikiwa ni ishara ya heshima kubwa kwa mchango wake unaokua kwa kasi katika tasnia ya muziki barani Afrika. Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa Rolling Stone Africa, waliandika: “Abigail Chams aingia kwenye mwangaza – Kutoka kwenye ala za hisia hadi mashairi ya Kiswahili, Abigail Chams anawaalika wasikilizaji katika mazingira ya sauti ambapo mila inakutana na ubunifu.” Jalada hilo linaonesha picha ya Abby akiwa na mtazamo wa kujiamini, akiwakilisha kizazi kipya cha wasanii wa Kiafrika wanaovuka mipaka kwa sauti, mitindo na ujumbe wao. Kutajwa kwake kama “Future of Music” ni uthibitisho wa upekee wa mtindo wake wa muziki unaochanganya ala za jadi, sauti za kisasa, na matumizi ya Kiswahili katika muziki wa kimataifa. Abby Chams, ambaye ameendelea kung’ara kwa nyimbo zake zenye ujumbe wa kina na ladha ya kipekee ya Afro-soul, ameonekana kuendelea kuvunja vizingiti, hasa kwa wasanii wachanga wa kike kutoka Afrika Mashariki. Mashabiki na wadau mbalimbali wa muziki wamempongeza Abby kwa hatua hiyo kubwa, wakisema kuwa huu ni mwanzo tu wa mafanikio makubwa zaidi.

Read More
 ABBY CHAMS AAHIDI KUFANYA MAKUBWA SONY MUSIC

ABBY CHAMS AAHIDI KUFANYA MAKUBWA SONY MUSIC

Mrembo mwenye kipaji kikubwa, Abby Chams ambaye amesaini mkataba na kampuni ya Sony Music Entertainment, amesema anajivunia kujiunga na lebo hiyo kubwa ya muziki kwani ndoto zake zinakwenda kutimia haraka. Akizungumza mara baada ya kusaini dili hilo Juni 8, 2022, Abigial amesema anajiona mwenye bahati na anaahidi kufanya makubwa kwani kazi yake inakwenda kuwa nyepesi chini ya Sony. “Najiona mwenye bahati ya kipekee kuwa mmoja wanafamilia wa lebo kubwa Afrika, ndoto zangu zimetimia, Ninaahidi kuwapa mashabiki wangu vitu vizuri zaidi,” alisema. Kwa upande wake mkuu wa Sony Music Afrika Mashariki, Christine ‘Seven’ Mosha, amesema anafahamu uwezo wa binti huyo mwenye sauti nzuri ya kuvutia mashabiki hivyo anafurahi kuwa naye. Mrembo huyo anatarajia kuachia wimbo wake mpya wa U and I Ijumaa hii, Juni 17.

Read More
 ABBY CHAMS ADAI CHANGAMOTO YA KUTONGOZWA NA MAPRODYUZA KARIBU IMFANYE AACHE MUZIKI

ABBY CHAMS ADAI CHANGAMOTO YA KUTONGOZWA NA MAPRODYUZA KARIBU IMFANYE AACHE MUZIKI

Msanii wa Bongofleva, Abby Chams anasema amepitia changamoto katika harakati zake kama msanii wa kike hasa katika mchakato wa uandishi wa muziki, kurekodi na kuhakikisha kwamba wimbo wake unasikizwa na umma. Abby anasema kwamba kwa miaka mingi tangu aanze safari ya muziki amekabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kutongozwa na watayarishaji wa muziki na waelekezi wa video. “Ukweli mimi kama mwanamuziki kwenye sekta hii zipo changamoto, unajua nina miaka 18 tu na unajua ninafanya kazi na watu wengi, Producers na Directors ni wakubwa sana kwangu- ni kama wazee, wananitongoza, Yaani wananiweka kwenye hali ambayo sio nzuri “, anasema. Msanii huyo ameiambia BBC kwamba tabia hiyo ilimkera sana hadi kulazimika kukataa uhusiano wa kibiashara na baadhi ya watu aliokuwa akifahamiana nao.

Read More