Rayvanny adokeza ujio wa kolabo nyingine na Abigail Chams
Bosi wa Label ya Next Level Music (NLM), Msanii Rayvanny ameingia tena studio kufanya kazi na Abigail Chams ikiwa ni baada ya mwaka mmoja. Rayvanny aliwahi kumshirikisha Abigail Chams katika wimbo wake ‘Stay’ unaopatikana kwenye EP yake, New Chui iliyotoka Oktoba mwaka 2021. Hatua hiyo inakuja baada ya hivi karibuni Abigail Chams kufanya nyimbo mbili na Harmonize, ambazo ni Closer na Leave Me Alone. Kwa sasa Rayvanny anafanya vizuri na wimbo wake ‘Nitongoze’ akimshirikisha Diamond Platnumz ukiwa ni wimbo wa nane kufanya pamoja.
Read More