Promota Abtex afunguka kutomsamehe Serena Bata

Promota Abtex afunguka kutomsamehe Serena Bata

Promota wa muziki kutoka nchini Uganda Abtex amefunguka kuwa hana mpango wa kumsamehe msanii serena bata licha ya msanii huyo kusimama naye kipindi anatoka gerezani. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni amesema bado ana machungu na serena kwa kuvunja mkataba wa kufanya naye kazi licha ya kuwekeza mamilioni ya pesa kusimamia muziki wake. “Niliwekeza zaidi ya milioni 300 kwa Serena. Nilikuwa na ndoto kubwa lakini alisambaratisha kila kitu nilipopata changamoto kadhaa. Alikimbia kwa mwanasheria na kuomba kuvunja mkataba wetu. Alianza kunifanyia mambo machafu.”, Alisema. Abtex amedai kuwa hivi karibuni atamchukulia hatua kali za kisheria msanii huyo ili aweze kulipa fedha zote alizotumia kugharamia muziki wake. “Kwa kweli, huwezi kucheza na pesa zangu hivyo. Ningekuwa nimejenga nyumba kwa pesa yangu lakini niliwekeza kwake. Nina maumivu makali na namchukia sana. Nitachukua hatua kali za kisheria hivi karibuni,” Abitex alielezea Utakumbukwa Promota Abtex alitoka jela kwa dhamana mapema wiki hii na Serena Bata alikuwa moja kati ya watu waliojitokeza kumpokea na kumuonyesha upendo. Wawili hao walifanya kazi pamoja lakini walivunja mkataba wao mwaka jana na wakaanza kuwa maadui. Kwa Serena, kwenda kusimama na Abitex wakati wa matatizo ilikuwa ni ishara kuweka kando tofauti zao, lakini kwa Abitex bado ana machungu na mrembo huyo.

Read More
 Abtex Promotions avunja mkataba na msanii Serena Bata.

Abtex Promotions avunja mkataba na msanii Serena Bata.

Meneja wa wasanii nchini Uganda Abbey Musinguzi maarufu Abtex Promotions ametangaza kusitisha kufanya kazi na msanii Serena Bata. Hii ni baada ya msanii huyo kuonekana akivuta sigara hadharani kitendo ambacho kilimkasirisha meneja wake huyo na kuchukua maamuzi magumu ya kutofanya naye kazi. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Abtex amesema licha ya kuvunja mkataba wake na Serena Bata, haitaathiri ratiba ya shows ambazo alikuwa amepangiwa na uongozi wake mwaka 2022. Ikumbukwe Serena Bata amekuwa chini ya uongozi wa Abtex Promotions kwa kipindi cha miaka miwili.

Read More
 PROMOTA ABTEX AZIDI KUMRUSHIA VIJEMBE PALLASO, ADAI TAMAA YA PESA ITAMPONZA KWENYE MUZIKI WAKE

PROMOTA ABTEX AZIDI KUMRUSHIA VIJEMBE PALLASO, ADAI TAMAA YA PESA ITAMPONZA KWENYE MUZIKI WAKE

Promota wa muziki nchini Uganda Abtex Musinguzi hana furaha kabisa na jinsi msanii Pallaso anasimamia shughuli zake za kibiashara. Kulingana na Abtex ,Pallaso pallaso na uongozi wake wamekuwa na mazoea ya kuchukua shows nyingi jambo ambalo limepelekea msanii huyo kushindwa kutumbuiza kwenye show zote ambazo amepewa. Promota huyo amemtaka Pallaso pamoja na uongozi wake aache tamaa ya pesa la sivyo wao kama mapromota watachukua maamuzi magumu ya kumaliza career ya Pallaso kwa kutompea michongo ya shows kwani msanii huyo anawavunjia mashabiki heshima kwa kususia shows. Utakumbuka juzi kati Pallaso alilazimika kufagia mji wa masaka kama njia ya kuwaomba mashabiki zake msamaha baada ya kuchelewa kufika kwenye perform yake  siku Wapendanao Duniani.    

Read More