Adasa akiri kupitia nyakati ngumu maishani

Adasa akiri kupitia nyakati ngumu maishani

Msanii wa muziki nchini Adasa amezua gumzo mtandaoni baada ya kufunguka kuwa amekuwa akipitia kipindi kigumu maishani mwake. Kupitia ukurasa wake wa Facebook mrembo huyo ameweka wazi kuwa hivi karibuni maisha yamekuwa yakimlemea japo tumaini lake bado liko kwa Mungu. Hata hivyo licha ya kutoeleza ni nini hasa kinachomsibu maishani, mashabiki zake wameonekana kumfariji kwa kumtumia jumbe za kumtia moyo.

Read More
 PRITTY VISHY ALIZWA NA KITENDO CHA ADASA KUTAKA KUMUIBIA MPENZI WAKE MSANII STIVO THE SIMPLE BOY

PRITTY VISHY ALIZWA NA KITENDO CHA ADASA KUTAKA KUMUIBIA MPENZI WAKE MSANII STIVO THE SIMPLE BOY

Mpenzi wa mwanamuziki Stivo The Simple, Pritty Vishy ameonekana kukerwa na kitendo cha msanii Adasa kuonekana kumzimia kimahaba rapa huyo kwenye moja ya video aliyoshare kwenye mtandao wa Instagram. Kwenye video hiyo ambayo wapo ufukweni mwa bahari Hindi, Adasa anaonekana akipiga stori na Stivo the Simple wakiwa matembezini ambapo ghafla aliaanza kumzungushia kiuno akiwa katika pozi la kimahaba zaidi, jambo ambalo lilimfanya Pritty Vishy ashuke kwenye uwanja wa comment ya post hiyo na kumpa Adasa somo akae mbali na mpenzi wake Stivo The Simple Boy, la sivyo atamfunza adabu. Hata hivyo Adasa alishindwa kumvumilia vitisho vilivyotolewa na mrembo huyo ambapo nae aliamua kujibu mapigo kwa kujitapa kwamba wakati Pritty Vishy kuwa na Stivo The Simple Boy kimahusiano ulishaisha kitambo, hivyo ni zamu yake kumuonesha msanii huyo mapenzi mujarab. Sasa baada ya kutunishiana misuli kwenye mtandao wa Instagram Prityy Vishy aliamua kwenda live instagram akiwa mwenye huzuni huku akiilaani vikali   kitendo cha Stivo the simple boy kumsaliti kimapenzi kwa kutoka na Adasa ambaye kwa mujibu amzidi na chochote. Hata hivyo hatua ya wawili hao kurushiana maneno makali hadharani kisa mwanaume imeibua hisia miongoni mwa walimwengu kwenye mitandao ya kijamii ambao wamehoji kuwa huenda wawili hao wanajaribu kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa kabla ya ujio wa ngoma mpya ya Stivo The Simple aliyomshirikisha Adasa.

Read More