Adidas yathibitisha Ronaldo hakugusa mpira kwenye mchezo wa Ureno dhidi ya Uruguay

Adidas yathibitisha Ronaldo hakugusa mpira kwenye mchezo wa Ureno dhidi ya Uruguay

Kampuni ya Adidas ametoa majibu ya utata wa Cristiano Ronaldo kwamba aliugusa au hakuugusa mpira ambao uliingia golini na Bruno Fernandes kutajwa kama mfungaji wa bao hilo kwenye mchezo wa Ureno dhidi ya Uruguay. Adidas wamesema Ronaldo hakuugusa mpira huo, Asante kwa kifaa maalum cha kuhisi (sensor) kilichopachikwa kwenye mpira huo unaotumika kwenye michuano hiyo ya Kombe la Dunia mwaka huu nchini Qatar. Timu ya Taifa ya Ureno imejihakikishia nafasi kwenye hatua ya 16 bora baada ya kupata ushindi wa 2-0 dhidi Uruguay kwenye mchezo wa kundi H Ureno inaongoza kwenye msimamo wa kundi H ikiwa imefikisha alama 6. Michezo ya mwisho itaamua timu itakayoungana na Ureno kwenye hatua ya mtoano katika kundi hilo lenye timu za Ghana na South Korea.

Read More
 Adidas kuendelea kuuza bidhaa za Yeezy

Adidas kuendelea kuuza bidhaa za Yeezy

Kampuni ya mitindo na mavazi Adidas imetangaza kuendelea kuuza bidhaa za rapa Kanye West “Yeezy” bila kutumia jina hilo. Siku ya jana kampuni hio ilitangaza kuachana rasmi na rapa huyo, baada ya kauli zake za chuki dhidi ya watu wa jamii ya kiyahudi. “Bidhaa zote za Yeezy zitauzwa chini ya jina la Adidas na zitatambulika kama bidhaa za Adidas” – Chanzo kutokea Adidas. Kampuni ya Adidas imeripotiwa kuwa itapoteza takribani shillingi millioni 30 mwaka huu kufuatia kuvunja uhusiano wake Kibiashara na Kanye West.

Read More
 Adidas yavunja mkataba na Kanye West

Adidas yavunja mkataba na Kanye West

Kampuni ya Adidas imeripotiwa kuvunja uhusiano wake wa kibiashara na Kanye West kufuatia kauli yake ya chuki dhidi ya Jamii ya Wayahudi. “Kampuni ya Adidas haivumilii hata kidogo maneno ya chuki na hatarishi kwa Umma yaliyotolewa na Kanye West. Kampuni imeamua kuvunja mkataba na Kanye West pamoja na kusitisha bidhaa zote zilizokuwa na ushirikiano pamoja na Yeezy” Imesomeka sehemu ya taarifa ya Adidas iliyotolewa kwa Umma. Itakumbukwa, tayari makampuni mengine kama Def Jam Records, Balenciaga na CAA yaliyokuwa yakifanya kazi na Kanye West, yashajiondoa kufanya nae kazi kufuatia sakata hilo la kauli za chuki.

Read More