Wizkid Aghairi Baadhi Matamasha Kufuatia Mauzo Duni ya Tiketi

Wizkid Aghairi Baadhi Matamasha Kufuatia Mauzo Duni ya Tiketi

Msanii nyota wa muziki wa Afrobeats, Ayodeji Balogun almaarufu kama Wizkid, ameripotiwa kughairi baadhi ya matamasha yake yaliyopangwa kufanyika katika kumbi mbalimbali barani Ulaya na Marekani, baada ya kukumbwa na changamoto ya mauzo duni ya tiketi. Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na waandaaji wa ziara hiyo, baadhi ya miji haikufikia viwango vya mauzo yaliyotarajiwa, hali iliyowalazimu waandaaji kufuta au kuahirisha baadhi ya tarehe zilizokuwa kwenye ratiba. Hata hivyo, wachambuzi wa tasnia ya burudani wanasema hali hii haipaswi kuchukuliwa kama dalili ya kuporomoka kwa kazi ya msanii huyo ambaye amewahi kushinda tuzo nyingi za kimataifa. “Changamoto ya mauzo ya tiketi inawakumba wasanii wengi kwa sasa, si Wizkid pekee. Hata Beyoncé alikumbwa na hali kama hii katika baadhi ya maeneo kwenye ziara yake ya hivi karibuni,” alisema mchambuzi wa burudani, Doreen Obasi. Kulingana na wachambuzi hao, kushuka kwa mauzo ya tiketi kunachangiwa na sababu mbalimbali, ikiwemo hali ya kiuchumi duniani, gharama ya juu ya maisha, pamoja na ushindani mkubwa katika ratiba ya burudani ya kimataifa. Licha ya hali hiyo, muziki wa Wizkid bado unaendelea kufanya vizuri kwenye majukwaa ya kidijitali kama Spotify na Apple Music, huku nyimbo zake zikisalia maarufu katika nchi nyingi za Afrika na diaspora. “Hatuwezi kupima mafanikio ya msanii kwa kigezo cha tiketi pekee. Wizkid bado ana ushawishi mkubwa katika muziki wa kimataifa,” aliongeza Obasi. Mashabiki wake wameshauriwa kutobadili mtazamo wao dhidi ya msanii huyo, kwani hali ya sasa inaweza kuwa ya muda tu, na tayari kuna juhudi zinafanywa kurekebisha mikakati ya usambazaji na utangazaji wa matamasha yajayo. Kwa sasa, Wizkid bado anatarajiwa kutumbuiza katika baadhi ya miji mikuu duniani ambako mauzo ya tiketi yamekuwa ya kuridhisha, huku akijipanga upya kwa msimu mpya wa burudani.

Read More
 Timaya: “Muziki Si Rahisi Tena, Wimbo Mmoja Unahitaji $100K

Timaya: “Muziki Si Rahisi Tena, Wimbo Mmoja Unahitaji $100K

Mwimbaji nguli wa muziki wa Afrobeats kutoka Nigeria, Timaya, amefichua changamoto kubwa inayowakumba wasanii katika sekta ya muziki, hasa linapokuja suala la kukuza kazi zao. Akiwa kwenye mahojiano ya hivi karibuni, Timaya alisema enzi zimebadilika sana, na kwamba mafanikio katika muziki kwa sasa yanahitaji uwekezaji mkubwa wa kifedha. Amefichua kuwa kwa sasa, msanii anayelenga kufanikisha wimbo mmoja kimafanikio, anahitaji bajeti isiyopungua dola 100,000 za Marekani. “To promote just one song, you need nothing less than $100k. That’s the world we live in now,” alisema Timaya kwa msisitizo. Mwanamuziki huyo ambaye alitamba na nyimbo kama “I Can’t Kill Myself,” “Balance” na “Cold Outside” aliweka wazi kuwa mafanikio hayategemei tena kipaji pekee, bali pia uwezo wa kifedha, mikakati ya kibiashara na nguvu ya usambazaji kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Kauli hiyo imezua mjadala mitandaoni, huku baadhi ya mashabiki wakikubaliana naye kwa kusema muziki wa sasa ni kama biashara nyingine yoyote, inayohitaji mtaji, ilhali wengine wakisema gharama hizo kubwa zinaweka vizingiti kwa vipaji vipya vinavyochipukia. Hata hivyo, Timaya amesisitiza kuwa ingawa njia ya mafanikio si rahisi, wasanii wanapaswa kujifunza kuweka mikakati ya kibiashara sambamba na ubunifu wao ili kufanikisha ndoto zao katika tasnia ya muziki.

Read More
 Ruger Afunguka Kuhusu Jeraha Lake la Kwanza la Kihisia Akiwa na Miaka 6 Tu

Ruger Afunguka Kuhusu Jeraha Lake la Kwanza la Kihisia Akiwa na Miaka 6 Tu

Mwanamuziki maarufu kutoka Nigeria, Ruger, amefunguka kuhusu tukio la kihisia lililomgusa sana alipokuwa na umri wa miaka sita tu. Akiwa mgeni katika kipindi cha The Bro Bants, msanii huyo alisimulia kwa uaminifu jinsi tukio hilo lilivyomwathiri na kumtengeneza katika safari yake ya maisha na mahusiano. Katika mahojiano hayo, Ruger alikumbuka kwa huzuni namna alivyomwona msichana aliyemuita mpenzi wake akiwa na mvulana mwingine. Tukio hilo lilimvunja moyo na kumuacha na jeraha la kwanza la kihisia, hata kabla hajakomaa kifikra kuelewa maana halisi ya mapenzi. “Nilikuwa na miaka sita tu,” alieleza Ruger. “Nilimpenda kweli yule msichana… lakini nikamkuta akicheza na kijana mwingine. Iliniuma sana, na tangu siku hiyo nikawa na tahadhari kubwa linapokuja suala la mapenzi.” Ruger alikiri kuwa uzoefu huo wa utotoni uliathiri namna anavyochukulia mahusiano hadi leo, akisema mara nyingi amekuwa mgumu kuamini watu kwa urahisi. Hata hivyo, aliongeza kuwa amejifunza kukua kutokana na maumivu hayo ya awali na kuyatumia kama msukumo katika sanaa yake ya muziki. Mashabiki wa Ruger wamekuwa wakimpongeza kwa ujasiri wa kusimulia hadithi hiyo ya kihisia, wakisema inaonyesha upande wa binadamu wa msanii huyo ambaye kwa kawaida hujulikana kwa sauti yake ya kipekee na midundo ya kuvutia.

Read More
 Davido Afichua: “Kama Sisingekuwa Msanii, Ningekuwa Mwandishi wa Habari”

Davido Afichua: “Kama Sisingekuwa Msanii, Ningekuwa Mwandishi wa Habari”

Msanii nyota wa Afrobeats kutoka Nigeria, Davido, amewashangaza mashabiki wake kwa kufichua kwamba angekuwa mwandishi wa habari kama hangejikita kwenye muziki. Kauli hiyo ya kushangaza ilitolewa wakati wa mahojiano ya moja kwa moja kwenye Beat 96.1FM, ambako msanii huyo alizungumza kwa undani kuhusu maisha yake nje ya jukwaa. Katika mahojiano hayo, Davido alieleza jinsi ambavyo kampeni ya kutangaza albamu yake mpya imekuwa ya kuchosha, lakini kwa upande mwingine, anafurahia sana mazungumzo na mikutano na wanahabari, tofauti na wasanii wengi wa kiwango chake.  “Nimekuwa nikifanya promo kali kwa ajili ya albamu yangu – si kazi rahisi. Sina haja ya kufanya promo lakini napenda. Napenda kuongea. Watu wengi hawajui kwamba mbali na kusomea usimamizi wa biashara, pia nimesomea masoko. Kwa hiyo napenda mazungumzo. Kama ningekuwa na podcast, ningeweza kuzungumza siku tatu au nne mfululizo.” Tofauti na wasanii wengi wanaoepuka kamera na mahojiano, Davido anaamini kuwa mazungumzo ni sehemu ya sanaa, na kwamba huwa anajihusisha sana na taarifa mbalimbali za kijamii na kisiasa. “Ni sehemu ya kuwa msanii, kwa mtazamo wangu. Si kila mtu hupenda kuzungumza, lakini mimi napenda. Nikikutana na mtu, napenda kuongea. Napenda habari. Ukiingia nyumbani kwangu, kila mara mimi huhakikisha kuna taarifa – huwezi kukosa CNN kwenye runinga ya sebuleni.” Akiendelea kufunguka, Davido alieleza kuwa mara nyingi akiwa nyumbani hujikuta akifanya utafiti kuhusu mambo mbalimbali, ishara kuwa ana kiu ya maarifa na kujua yanayoendelea duniani. Kwa msingi wa mapenzi yake makubwa kwa mawasiliano, Davido alisema kwamba kama hangekuwa msanii, basi angekuwa mtangazaji au mwanahabari. “Mimi ni mtu ninayependa taarifa. Naona kama nisingekuwa kikamilifu kwenye muziki, basi ningekuwa kwenye kitu kama uandishi wa habari. Napenda kuwaeleza watu kile ninachofanya.” Aidha, alizungumzia kuhusu umaarufu wake mitandaoni, akisema kuwa sababu mojawapo ni kujishughulisha, kushiriki, na kuwasiliana moja kwa moja na mashabiki wake. “Watu huuliza kwa nini nina followers wengi – ni kwa sababu najihusisha na watu, na ninafanya kazi kila wakati.” Kwa kauli zake, Davido anaonesha kuwa yeye si msanii wa kawaida tu, bali ni msomi wa mawasiliano, mpenzi wa taarifa, na mtu anayeamini kuwa muziki na mawasiliano vinaenda pamoja. Hali hii huenda ikamfungulia milango ya vipindi vya podcast au mahojiano ya runinga siku za usoni.

Read More