Happy C aumizwa na hatua ya Akeelah kuacha muziki.

Happy C aumizwa na hatua ya Akeelah kuacha muziki.

Msanii kutoka 001 music Happy C ameoneshwa kusikitishwa na kitendo cha Akeelah kutangaza kuacha muziki. Kwenye mahojiano na Captain Nyota amesema Akeelah ni msanii mwenye kipaji cha kipekee kwenye muziki wa Kenya, hivyo hapaswi kukata tamaa kwenye harakati za kuipambania ndoto yake kwa kuwa muziki una changamoto nyingi. Happy C amemshauri kujifikiria tena kutokana na maamuzi magumu ambayo ameyachukua kwenye muziki wake na atumie changamoto kama kigezo cha kufanya makubwa. Kauli yake imekuja baada ya Akeelah kusema ameamua kuacha muziki kwa sababu ya maonevu na unyanyasaji alioupitia katika safari yake ya mziki. Hitmaker huyo wa Tujikumbushe, alienda mbali Zaidi na kuushukuru uongozi wa Hakim Empire kwa mchango wao kwake huku akikosa kuutaja uongozi wa Shirko Media ambao ulimlea kimziki.

Read More
 Akeelah atangaza kuacha muziki

Akeelah atangaza kuacha muziki

Msanii wa kike kutoka Kenya Akeelah amezua gumzo mtandaoni baada ya kutangaza kuwa ameacha muziki kabisa. Kupitia insta story yake Akeelah ameandika kuacha muziki kwa sababu ya maonevu na unyanyasaji alioupitia katika safari yake ya mziki. Hitmaker huyo wa Tujikumbushe, ameushukuru uongozi wa Hakim Empire kwa mchango wao kwake huku akikosa kuutaja uongozi wa Shirko Media ambao ulimlea kimziki. Akeelah hata hivyo ameondoa picha zake zote kwenye akaunti yake ya instagram, hii imeleta maswali na hisia kwa mashabiki zake kuwa inawezekana msanii huyo yupo mbioni kuachia kazi mpya za muziki.

Read More