Mwakideu Asema Hakujua Dada Yake Atafichua Siri za Ndoa Yake na Burale

Mwakideu Asema Hakujua Dada Yake Atafichua Siri za Ndoa Yake na Burale

Mtangazaji maarufu wa redio, Alex Mwakideu, amekanusha madai kwamba alimpangia mtego mhubiri na mtangazaji Robert Burale kwenye kipindi chake cha podcast, baada ya mahojiano yaliyosababisha gumzo kubwa mitandaoni. Tuhuma hizo zilijitokeza baada ya Rozinah Mwakideu, dada yake Alex, kuibua mjadala mkali kwa kufichua kuwa kuolewa na Burale ilikuwa kosa kubwa zaidi maishani mwake. Kauli hiyo ilitolewa wiki moja tu baada ya Burale mwenyewe kuonekana kwenye podcast hiyo, jambo lililoibua hisia kuwa Alex aliratibu mahojiano hayo makusudi ili kumuaibisha Burale. Hata hivyo, kupitia kauli yake kwa vyombo vya habari, Alex alieleza kuwa hakuwa na ufahamu wowote kuhusu kile ambacho dada yake alipanga kusema, na alibaini maoni yake kwa mara ya kwanza wakati wa mahojiano hayo hewani. Mwakideu alisisitiza kuwa kipindi hicho hakikuwa mtego wala jaribio la kumvuta Burale kwenye mjadala wa kifamilia, bali ni sehemu ya mahojiano ya kawaida yanayolenga kushirikisha watu wenye hadithi tofauti za maisha. Aliongeza kuwa kufanana kwa muda wa mahojiano hayo kulikuwa ni “bahati mbaya tu, si mpango wa makusudi.” Tukio hilo limezua mjadala mkubwa mitandaoni, huku baadhi ya mashabiki wakimtetea Mwakideu kwa uwazi wake, na wengine wakidai kwamba angepaswa kuwa makini zaidi kuepuka mahojiano yanayohusisha masuala ya kifamilia.

Read More
 Watangazaji wa Radio 47 Wamchana Bahati kwa Kauli ya Kununua Kituo Chao

Watangazaji wa Radio 47 Wamchana Bahati kwa Kauli ya Kununua Kituo Chao

Watangazaji maarufu wa Radio 47, Alex Mwakideu na Emmanuel Mwashumbe, wamemtolea uvivu msanii Bahati kufuatia kauli yake kwamba angeweza kununua kituo cha Radio 47 pamoja na TV47 na kisha kumpa mke wake, Diana Marua, nafasi ya ubosi ili amsimamie mtangazaji Fred Arocho. Katika kipindi cha asubuhi cha kituo hicho leo, Mwakideu na Mwashumbe walionekana kukerwa na matamshi ya Bahati, wakimtaka aache kujisifu na kudanganya mashabiki wake kuhusu uwezo wake kifedha. Walisema kuwa madai ya Bahati ni ya uongo kwani hana uwezo wa kununua kampuni ya Cape Media, wamiliki wa Radio 47 na TV47. Kauli ya Bahati ilikuja baada ya Arocho kumshinikiza kutimiza ahadi yake ya shilingi milioni moja aliyoitoa kwa Harambee Stars. Msanii huyo alijibu kwa kejeli akidai kwamba akikasirika anaweza hata kununua kituo hicho na kumfanya Diana Marua kuwa bosi wa Arocho. Hata hivyo, watangazaji hao walisema maneno ya Bahati hayana msingi, wakimtupia vijembe kwamba kama kweli ana uwezo huo, basi aanze kwanza kwa kumudu mishahara yao. “Wee huna pesa! Usiwadanganye watu,” waliongeza kwa dhihaka, wakimshauri aendelee na kazi yake ya muziki badala ya kuingilia masuala ya vyombo vya habari. Hali hii imezua gumzo mitandaoni, huku mashabiki wakigawanyika kati ya wanaomuunga mkono Bahati na wale wanaosema amejipata pabaya baada ya kuwakera watangazaji wenye ushawishi mkubwa.

Read More