Mwigizaji Mtandaoni Am Kabugi Akanusha Taarifa za Kupatwa na Msongo

Mwigizaji Mtandaoni Am Kabugi Akanusha Taarifa za Kupatwa na Msongo

Mwigizaji wa mtandaoni, Am Kabugi, amekanusha taarifa zinazoenea mitandaoni kuwa anapitia changamoto za msongo wa mawazo kutokana na hali ngumu ya maisha jijini Nairobi. Kupitia Insta Story yake, Kabugi amefafanua kuwa hana tatizo la msongo wa mawazo kama inavyodaiwa, bali anatafakari uwezekano wa kuhamia miji mingine mikubwa kama Nakuru, Kisumu, Mombasa, au Eldoret ambako anaamini maisha yanaweza kuwa nafuu zaidi. Msanii huyo kutoka Kenya, ameongeza kuwa kauli yake kuhusu maisha ya Nairobi haikumaanisha kwamba amelemewa kimaisha, bali ilikuwa ni njia ya kuonesha jinsi gharama ya maisha jijini Nairobi inavyozidi kuongezeka kila siku. Hii ni baada ya mapema leo kutoa kauli kwamba maisha jijini Nairobi yamekuwa magumu, hali iliyotafsiriwa na baadhi ya mashabiki kuwa huenda anaathirika kisaikolojia.

Read More