Amber Lulu aumizwa vibaya kwa vipigo

Amber Lulu aumizwa vibaya kwa vipigo

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Amber Lulu ameweka wazi changamoto anazozipitia katika mahusiano yake ikiwa ni pamoja na kupigwa na kutishiwa kuuawa. Kupitia instastory yake mrembo huyo ameandika ujumbe mrefu wa masikitiko akieleza namna alivyoumizwa vibaya kwa kipigo huku akidai sababu kubwa ya kupitia manyanyaso hayo ni mtoto wake. “Daa nimekuwa mtu wakuangaika na kuteseka pasipo sababu ya msingi. Kuna muda natamani kumkumbatia mwanangu nishinde nae nashindwa ‘coz’ nisipo hangaika mwanangu atakula nini?..Nyumba nalipa nini? Leo napigwa kama mbwa kisa kumuhangaikia Mwanangu naumia sahivi mtu ananitishia kuniuaa Mungu”…Aliandika.

Read More
 AMBER LULU APOKEZWA TUZO YA SILVER PLAY BUTTON NA MTANDAO WA YOUTUBE

AMBER LULU APOKEZWA TUZO YA SILVER PLAY BUTTON NA MTANDAO WA YOUTUBE

Msanii wa Bongofleva Amber Lulu ametunukiwa tuzo ya Silver Play  Button na mtandao wa youtube baada ya kufikisha jumla ya subscribers laki moja kwenye chanel yake. Amber Lulu ametumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kuwashukuru mashabiki zake kwa upendo ambao wanazidi kumuonyesha kupitia kazi zake za muziki huku akiahidi kuendelea kuwapa burudani zaidi. “Asanteni sana my fans asanteni you tube kwa zawadii ni hatua nzur katika safar yangu ya mziki naomba muendelee ku subscribe thanx 🙏,” Ameandika kupitia Instagram Channel ya youtube ya Amber Lulu ilifunguliwa rasmi Disemba 27 mwaka wa 2016 na mpaka sasa imefikisha zaidi ya watazamaji millioni 9.7 huku ikiwa na jumla ya subscribers 103, 000. Itakumbukwa tuzo ya silver play button huwa inatolewa kwa wanamuziki au watu maarufu kwenye mtandao wa youtube ambao hujizolea zaidi ya subcribers laki moja.

Read More
 AMBER LULU: NAMTAMANI SANA JUX

AMBER LULU: NAMTAMANI SANA JUX

Msanii wa Bongofleva Amber Lulu amemtaja Juma Jux kuwa ndio mwanaume anayetamani kupata naye mtoto kwa sababu ana akili, yupo smart na atamuongoza vyema lakini pia amekuwa akimfuatilia msanii huyo kwa muda mrefu. Mrembo huyo ambaye anafanya poa na singo yake mpya iitwayo Nimeachika amesema amepanga kuzaa watoto 5 kila mmoja na baba yake sababu akizaa na baba mmoja kisha akafariki yeye ataishia kupata tabu na watoto. Ikumbukwe pia Amber Lulu kipindi cha nyuma alishaweka wazi kutamani kuwa kwenye mahusiano na Diamond Platnumz, lakini hata hivyo nafasi ya kuwa na Diamond inaonekana ni nyembamba sababu baada ya hitmaker huyo wa Naanzaje kuzaa watoto 4 na wanawake tofauti amekiri hivi karibuni kuwa kwa sasa kuwa kwenye mahusiano na wanawake sio kipaumbele chake bali nguvu amezielekeza kwenye kuzidi kufanya kazi ili kuendelea kufanikiwa kiuchumi.

Read More