Amber Rose Aibua Mjadala Mpya Kuhusu Kesi ya Megan Thee Stallion

Amber Rose Aibua Mjadala Mpya Kuhusu Kesi ya Megan Thee Stallion

Mwanamitindo na mwanaharakati Amber Rose ameeleza hadharani sababu za kumtetea msanii Tory Lanez katika kesi ya kumpiga risasi Megan Thee Stallion mwaka 2020. Akizungumza kwenye mahojiano ya moja kwa moja katika kipindi cha Chris Cuomo kinachorushwa kupitia NewsNation, Rose alisema anaamini Lanez hana hatia na anastahili kusamehewa na Gavana wa California, Gavin Newsom. Katika mazungumzo hayo, Amber Rose alisisitiza kuwa ushahidi uliopo hauonyeshi moja kwa moja kuwa Tory ndiye alifyatua risasi. Alisema Lanez ameshathibitishwa kuwa hana uhusiano wa moja kwa moja na silaha iliyotumika, jambo linaloonyesha kuwa alipaswa kuachiliwa huru. Chris Cuomo, hata hivyo, aliibua hoja kuwa sampuli za DNA zilionyesha kuwa silaha hiyo ilikuwa inaweza kuguswa na watu wanne tofauti, lakini pia akaongeza kuwa Lanez alituma ujumbe wa kuomba msamaha baada ya tukio hilo, huku Megan Thee Stallion na rafiki yake Kelsey, waliokuwepo usiku huo, wakimtaja Lanez kama mtu aliyefyatua risasi. Amber Rose alijibu kwa kusema kuwa amesikia simulizi nzima kutoka kwa Tory Lanez mwenyewe, ambaye alimpigia simu moja kwa moja kutoka gerezani na kumueleza kile kilichotokea usiku huo. Kauli hii ya Amber Rose imezua maoni mseto mitandaoni, huku baadhi wakimtetea kwa kuonyesha huruma na kutaka haki ya kweli itendeke, huku wengine wakimtuhumu kwa kupuuza ushahidi wa upande wa Megan Thee Stallion. Haya yanakuja siku chache baada ya Amber Rose kuchapisha kipande cha video kinachomuonyesha Mwakilishi wa Bunge la Marekani, Anna Paulina, akimwambia Cuomo kuwa Tory Lanez hana hatia na kwamba kesi hiyo ililetwa kwake na Amber Rose mwenyewe.

Read More
 Amber Rose mbioni kuandika kitabu kuhusu dhuluma dhidi ya wanawake

Amber Rose mbioni kuandika kitabu kuhusu dhuluma dhidi ya wanawake

Mwanamitindo maarufu duniani Amber Rose ameibuka na kudai kuwa kuna unyanyasaji mkubwa sana wa wanawake lakini vyombo vya habari vimekuwa na upendeleo pale mwanamke anapojitokeza kuongea ukweli. Amber amefunguka kuwa ndio maana huchukua miaka mingi kwa mwanamke kuja kuzungumza unyanyasaji alioupitia kwenye maisha yake kwani wakijitokeza mapema huitwa waongo. Mwanamama huyo ambaye kipindi cha nyuma aliwahi kuwa kwenye mahusiano na Rapa Kanye West, ameahidi kuandika kitabu kwani hawezi kufunguka yote kupitia mitandao ya kijamii. Lakini pia amesema atachangia wale wote waliothirika na dhuluma za kijinsia.

Read More
 AMBER ROSE AFUNGUKA SAKATA LA KANYE WEST NA NICKI MINAJ KUPITIA WIMBO WA MONSTER

AMBER ROSE AFUNGUKA SAKATA LA KANYE WEST NA NICKI MINAJ KUPITIA WIMBO WA MONSTER

Verse ya Nicki Minaj kwenye ngoma ya Kanye West “Monster” ya mwaka 2010 ilikuwa ya moto sana ingawa YE hajawahi kufurahishwa na mauaji ya mrembo huyo kwenye ngoma hiyo. Sasa Amber Rose ambaye ndiye alimleta Nicki Minaj studio kuifanya verse hiyo, amerudi tena na kufunguka mengi kuhusu sakata hilo. Kwenye mahojiano yake na Podcast ya (Higher Learning) Amber amesema Kanye West aliwahi kumtamkia wazi kuwa, kwanini umeniletea mtu ambaye amekuja kuniua kwenye ngoma yangu? YE: “How the f*ck did you bring in a b*tch that killed me on my own song?” Amesema. Utakumbuka mwanamitindo na mwigizaji kutoka Marekani Amber Rose aliwahi kukaririwa mwaka 2018 akisema YE alibaki kidogo aifute verse hiyo.

Read More
 AMBER ROSE AFUNGUKA KUHUSU TWEET YAKE  YA MWAKA 2015 INAYOONEKANA KUMPONZA EX WAKE KANYE WEST

AMBER ROSE AFUNGUKA KUHUSU TWEET YAKE YA MWAKA 2015 INAYOONEKANA KUMPONZA EX WAKE KANYE WEST

Mwanamitindo kutoka Marekani, Amber Rose amevunja kimya chake kuhusu sakata linaloizingira ndoa ya  Kim Kardashian na Kanye West baada ya watu kumkumbusha tweet yake ya zamani aliyomponda Kanye West. Tweet hiyo aliyoipost mwaka 2015 baada ya kuachana na Kanye West ilisomeka  “Kanye West, nitawaachia ‘Kartrashians’ wakudhalilishe pale ambapo watakuwa wamemalizana na wewe.” Hiyo ilikuwa baada ya Kanye West kufanya mahojiano na kituo cha break fast club na kusema kuwa ilimbidi aoge mara 30 kabla ya kukutana na familia ya The Kardashians kutokana na uchafu wa aliyekuwa Ex wake Amber Rose. Baada ya mashabiki kumkumbusha tweet yake hiyo katika hali ya kumbeza Kanye West ambaye amekuwa akipitia wakati mgumu kutoka kwa familia ya Kim, Amber Rose ameibuka na kusema tweet hiyo ilikuwa ni ya zamani na kwa sasa alishajifunza kutokana na makosa yake, hivyo hawezi kuingilia maisha ya familia yeyote na The Kardashians hawakutakiwa kuambiwa maneno kama yale. Utakumbuka Amber rose na Kanye west walikuwa kwenye mahusiano kati ya  mwaka 2008 na 2010 lakini walikuja wakaachana baada kanye west kuingia kwenye mahusiano na baby mama wake kim kardashian

Read More