Azeezah Hashim Asema Wanaume Wanaomfuata Andrew Tate au Kibe ni Red Flag

Azeezah Hashim Asema Wanaume Wanaomfuata Andrew Tate au Kibe ni Red Flag

Mtangazaji na mrembo maarufu Azeezah Hashim amezua gumzo mitandaoni baada ya kueleza msimamo wake kuhusu wanaume wanaoamini na kufuata mitazamo ya wanablogu wenye utata Andrew Tate na Andrew Kibe. Katika mahojiano na Milard Ayo, Azeezah alisema wazi kuwa hawezi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanaume anayeshikilia imani kwamba wanaume na wanawake hawawezi kuwa marafiki au wenza wa kweli. Alisisitiza kuwa uhusiano bora hujengwa kwa heshima, maelewano, na upendo wa kweli si kwa nguvu au ubabe wa kijinsia. “Mimi nahitaji mwanaume ambaye anaonyesha upendo wa kweli, siyo mtu anayefikiri kwamba wanawake ni wa kutumia au wa kuwatawala. Ukiniambia unaamini itakadi kama za Andrew Tate au Kibe, hiyo ni red flag ya kwanza na ya mwisho,” alisema Azeezah kwa msisitizo. Kauli hiyo imezua mijadala mitandaoni huku baadhi ya watu wakimpongeza kwa kusimamia maadili ya heshima kwenye mahusiano, huku wengine wakikosoa mtazamo wake wakidai kila mtu ana uhuru wa kufuata kile anachoamini. Andrew Tate na Andrew Kibe ni majina yanayojulikana kwa kutoa mitazamo mikali kuhusu jinsia, ambayo kwa sehemu kubwa imekuwa ikipingwa na watu wanaotetea usawa wa kijinsia.

Read More
 Andrew Kibe Afichua Siri ya DMs za Director Trevor, Akanusha Kuomba Msaada

Andrew Kibe Afichua Siri ya DMs za Director Trevor, Akanusha Kuomba Msaada

Mtangazaji na mwanahabari maarufu Andrew Kibe amevunja ukimya na kujibu madai yanayomhusisha na Director Trevor, akisema kuwa taarifa kwamba aliwahi kumwomba msaada si za kweli. Kibe anasema kwa uwazi kuwa ni Trevor ndiye aliyekuwa akimtafuta mara kwa mara kupitia ujumbe wa moja kwa moja (DMs) alipokuwa Marekani, kipindi ambacho Trevor alikuwa bado kwenye uhusiano na Mungai Eve. Kwa mujibu wa Kibe, Trevor alikuwa akimuomba msaada wa kumsadia kufungua upya ukurasa wake wa Facebook, na sasa anamtaka aweke wazi jumbe hizo kwa umma ili ukweli ujulikane. “Ningependa Trevor aonyeshe jumbe alizoniandikia wakati akinitafuta msaada. Aache kupotosha watu,” alisema Kibe kwa msisitizo. Mbali na hayo, Kibe amemkosoa Trevor kwa kile alichokitaja kama tabia ya kutafuta umaarufu wa haraka (clout) kwa kutumia majina ya watu maarufu. Amemshauri aweke kando drama zisizo na msingi na ajikite kwenye kazi halali zitakazompa heshima na mafanikio ya kweli. Pia, amemwonya kuhusu kuweka mahusiano kwenye mitandao, akisema hatua hiyo huweza kuishia kwa fedheha kama ilivyotokea kwa msanii Mulamwah. Kauli hiyo ya Kibe imejibu shutuma zilizotolewa awali na Trevor, aliyedai kuwa Kibe alimdhalilisha kwa kumuita “mwanaume asiyekuwa na msimamo na aliyekaliwa na mwanamke”, kufuatia kuvunjika kwa mahusiano yake na Mungai Eve. Trevor alisema maneno hayo yalimuumiza kihisia na kudhoofisha heshima yake binafsi. Hata hivyo, Trevor amesema amepitia mengi, lakini kwa sasa amepona kihisia, amejijenga upya, na anaendelea kujiimarisha kimaisha na kitaaluma. Amedai kuwa licha ya changamoto alizopitia, ameibuka kuwa mtu mpya mwenye maono mapya. Mvutano huu kati ya wawili hao maarufu umechochea mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, huku mashabiki wakiwa wamegawanyika kati ya wanaomuunga mkono Kibe na wale wanaompigia debe Trevor. Wapo wanaosema drama hii ni ya kutafuta kiki, huku wengine wakitaka wahusika waache tofauti zao na wajikite kwenye kazi.

Read More
 RINGTONE AMCHANA ANDREW KIBE KISA NDOA YA MWANAMUZIKI WA NYIMBO ZA INJILI GUARDIAN ANGEL

RINGTONE AMCHANA ANDREW KIBE KISA NDOA YA MWANAMUZIKI WA NYIMBO ZA INJILI GUARDIAN ANGEL

Msanii wa nyimbo za injili nchini Ringtone amemtolea uvivu mwanahabari mwenye utata nchini Andrew Kibe kwa madai ya kuikosoa ndoa ya msanii Guardian Angel na mke wa Esther Musila. Kupitia instagram page yake Ringtone amemtaka kibe aheshimu maamuzi ya Guardian Angel na mke wake Esther Musila kuhalilisha ndoa kwa njia ya harusi ikizingatiwa kuwa ni watu wazima ambao upendo uliwaleta pamoja licha ya utofauti wa umri wao. Hitmaker huyo wa “Sisi ndio tuko” ameenda mbali na kumshauri Kibe akome kuingilia maisha ya wana ndoa hao wawili na badala yake aelekeze nguvu zake kwenye shughuli itakayomuingizia kipato kwani anapoteza muda wake kuzungumzia jambo ambalo litamsaidia maishani. Kauli ya Ringtone imekuja mara baada ya Andrew Kibe kuonekana kukejeli ndoa ya Guardian Angel na mke wake Esther Musila kwa kusema kwamba haoni ndoa hiyo ikidumu kwani msanii huyo aliwavunjia heshima vijana wa Kenya kwa hatua kumuoa mwanamke mkubwa kiumri.

Read More