ANGELINA AKANUSHA TAARIFA ZA KUWA MJA MZITO

ANGELINA AKANUSHA TAARIFA ZA KUWA MJA MZITO

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Angelina amekanusha madai yanayotembea kwenye mitandao ya kijamii kuwa ni mja mzito. Katika mahojiano yake hivi karibuni Angelina amesema ameshangazwa na hatua ya watu kumtumia jumbe za kumtakia kheri ya kupata uja uzito licha ya kutokuwa na uja uzito wowote. Angelina amesema taarifa za yeye kuwa mja mzito zimechangiwa na namna ambavyo amebadilika kimwili na picha ambazo pia amekuwa akizichapisha kwenye mitandao yake ya kijamii, jambo ambalo amedai liliwaaminisha walimwengu kuwa huenda mrembo huyo ana-edit sana picha zake kuficha uja uzito. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Go Down” amesema hana mpango wa kupata uja uzito kwa sasa ila ameamua kuelekeza nguvu zake zote kwenye muziki wake hivyo mashabiki watarajie kazi nzuri kutoka kwake.

Read More
 ANGELINA ATANGAZA KUACHA MUZIKI

ANGELINA ATANGAZA KUACHA MUZIKI

Nyota wa muziki nchini uganda Angelina amedokeza mpango wa kuachana kabisa na masuala ya muziki. Angelina ameweka wazi hayo kupitia ukurasa wake wa twitter ambapo amesema ataacha muziki mwaka wa 2022 baada ya kuachia project yake ya mwisho ambayo amekuwa akiifanyia kazi kwa muda. Kulingana na mrembo huyo baada ya kuacha muziki ataelekeza nguvu zake kwingine katika suala zima la kujitafutia riziki. Hata hivyo tweet yake hiyo haikukaa kwa muda kwenye ukurasa wake twitter kwani alikuja akaifuta baada ya kuchapisha. Angelina amekuwa kwenye kiwanda cha muziki nchini Uganda kwa muda wa miaka kumi na ametoa hits kali kama Go Down, Ghetto Lovin, Ronaldo na nyingine kibao.

Read More