ANGELLA KATATUMBA AKIRI KUTESWA NA MAPENZI
Mwanamuziki kutoka uganda Angella Katatumba amewashangaza mashabiki wake alipofichua kwamba kuna kipindi maishani mwake alikula tu vipande vya barafu kwa takriban wiki tatu. Katika mahojiano yake hivi karibuni msanii huyo wa Black Market Records (BMR) amefunguka kuhusu matatizo yake ya maisha akisema kwamba alikula vipande vya barafu kwa wiki tatu alipoachwa na mume wake wa zamani nchini Marekani. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Wendy” amesema kwamba alipoachwa, alikuwa amefulia kiuchumi na hakuwa kitu cha kufanya ila kula tu vipande vya barafu. Angella katatumba ameenda mbali zaidi na kusema kwamba aliogopa hata kuwapigia simu wazazi wake nyumbani kwa ajili ya kuomba msaada wa kifedha kwa kuwa aliona aibu juu kuachwa na mume wake. Hata hivyo amesema anamshukuru Mungu kwa kumfanya ashinde hali ngumu aliyokuwa akipitia kipindi hicho ingawa alipoteza takriban kilo 38 kwa wiki tatu alizokuwa anakula vipande vya barafu.
Read More