Msanii Anjella Aingia Rasmi Kwenye UdalaIi wa Nyumba Baada ya Kushindwa na Muziki
Mwanamuziki wa Bongofleva Anjella ameibuka na kuweka wazi kuwa maisha ya sanaa yamekuwa magumu kwake, hasa upande wa kupata kipato cha kutosha, hali iliyomlazimu kuanza kutafuta riziki kupitia udalali wa nyumba. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Anjella amesema wazi kuwa muziki haujamletea mapato ya kutosheleza mahitaji yake, na hivyo ameamua kuwekeza nguvu katika kazi ya udalali. Amesema hatua hiyo ni njia ya kujiongezea kipato na kujitegemea zaidi. Msanii huyo tayari ameonyesha kuwa amechukulia jambo hilo kwa umakini baada ya kuposti nyumba zinazopangishwa, akitoa taarifa kamili kwa wanaohitaji makazi. Anjella amewaomba madalali wenzake kumkaribisha kwenye magroup yao ili kufanya kazi kwa ushirikiano. Hatua yake imepata mwitikio mseto mtandaoni, huku baadhi ya mashabiki wakimsifu kwa ujasiri wa kutafuta riziki na wengine wakieleza kuwa hali ya wasanii wengi barani Afrika inahitaji kuboreshwa ili wapate manufaa zaidi kupitia kazi zao
Read More