Nicki Minaj Apata Msaada wa Kisiasa Kufuatia Vitisho vya MackWop

Nicki Minaj Apata Msaada wa Kisiasa Kufuatia Vitisho vya MackWop

Mbunge wa Marekani Anna Paulina Luna amethibitisha kuwa amewasiliana moja kwa moja na msanii wa rapa Nicki Minaj baada ya kauli za kutishia usalama wake kutolewa na MackWop, mshirika wa lebo ya TDE. Hatua hiyo imechukuliwa kama sehemu ya kuhakikisha usalama wa Minaj kufuatia matamshi ambayo yalionekana kama tishio la moja kwa moja dhidi ya maisha yake. Kauli ya MackWop, iliyotolewa kupitia livestream, ilieleza kuwa Minaj asipojichunga anaweza kuishia kama rafiki yake anayedhaniwa kuwa ni Tory Lanez, ambaye aliripotiwa kudungwa visu akiwa gerezani. Kauli hiyo imeibua hofu na taharuki miongoni mwa mashabiki na wanasiasa, na kuchochea mjadala kuhusu usalama wa wasanii katika tasnia ya burudani. Chanzo cha mvutano huu kilianza baada ya Minaj kuonyesha dhamira ya kufichua maovu aliyotendewa na MackWop wakati walipokuwa wakifanya kazi pamoja. Hatua hiyo haikupokelewa vyema na meneja huyo wa zamani, hali iliyochochea kauli za vitisho na mashambulizi ya maneno mtandaoni. Katika mkondo huo huo wa sintofahamu, msanii SZA pia alijikuta akihusishwa na ugomvi huo baada ya kuonekana kama anamrushia vijembe Minaj kupitia mafumbo kwenye mitandao ya kijamii. Minaj hakusita kumjibu kwa matusi na maneno makali, hali iliyoongeza moto katika mvutano huo wa hadharani. Mbunge Luna, akielezea msimamo wake, amesema kuwa vitisho vya aina hii haviwezi kufumbiwa macho, na ametoa hakikisho kuwa hatua zitachukuliwa ili kulinda wasanii dhidi ya ukatili wa kimfumo ndani ya tasnia ya muziki. Wito umetolewa kwa wadau wa muziki kuhakikisha mazingira salama, huru na ya haki kwa kila msanii bila woga wa kulipiziwa kisasi.

Read More