Annastacia Mukabwa afunga ndoa  na mpenzi wake wa siku nyingi Maurice William Juma

Annastacia Mukabwa afunga ndoa  na mpenzi wake wa siku nyingi Maurice William Juma

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Annastacia Mukabwa, amefunga ndoa  na mpenzi wake wa siku nyingi Maurice William Juma . Taarifa hizo zimethibitisha na marafiki zake wa karibu baada ya kuachia picha za baadhi ya matukio ya Harusi yao ambayo ilifanyika katika Kanisa Kuu la Praise huko Imara Daima, Nairobi Desemba 10. Harusi hiyo ilihudhuriwa na waimbaji kadhaa mashuhuri wa nyimbo za Injili, akiwemo Evelyne Wanjiru, Lady Bee na Solomon Mkubwa. Hata hivyo mastaa mbali mbali na mashabiki wake wamempongeza kwa hatua hiyo huku wakimtakia mema  na mume wake  katika safari yao ya ndoa.

Read More
 ANNASTACIA AJITAPA WIMBO WAKE NDIO CHANZO CHA RINGTONE KUACHA MUZIKI.

ANNASTACIA AJITAPA WIMBO WAKE NDIO CHANZO CHA RINGTONE KUACHA MUZIKI.

Mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini Annastacia Mukabwa, amefunguka kwa mara ya kwanza baada msanii mwenzake Ringtone Apoko kutangaza kuacha muziki wa injili. Katika mahojiano yake hivi karibuni Mukabwa amesema wimbo wake uitwao Kaa Kando ndio umempelekea Ringtone kuchukua maamuzi magumu ya kuacha muziki wa injili kwa sababu amekuwa akitumiwa na shetani kuichafua tasnia ya muziki huo nchini. “After releasing this Song Kaa Kando naona watu waliokuwa wamejificha ndani ya Gospel industry as Gospel artist wameanza kukaa Kando,” Amesema. “Wanatumiwa na shetani kuchafua sifa ya injili. Mungu anawaanika mmoja baada ya mwengine,” Ameongeza. Kauli yake imekuja mara baada ya Ringtone Apoko kudai kuwa wanawake waliokuwa wanamtaka kimapenzi ndio walimfanya akaacha muziki wa injili ambapo alienda mbali zaidi na kuwashauri wamfuate Yesu Kristo.  

Read More