Apple Yazindua iPhone 17, iPhone 17 Pro na iPhone Air
Kampuni ya Apple imezindua rasmi simu mpya ya iPhone 17, ambayo japokuwa muonekano wake unafanana na iPhone 16, imeboreshwa kwa kiwango kikubwa upande wa teknolojia. Sasa inakuja na skrini ya ProMotion inayowezesha refresh rate hadi 120Hz, badala ya 60Hz ya toleo lililopita. Pia, ina kamera kuu ya 48MP, kioo cha Ceramic Shield 2 kilichoimara zaidi dhidi ya michubuko na ajali, pamoja na teknolojia mpya ya kuchaji haraka. Kwa upande mwingine, Apple imezindua pia iPhone 17 Pro, ikiwa na mabadiliko makubwa zaidi. Toleo hili linatumia heat-forged aluminium badala ya titanium, na muundo wa kamera ya nyuma umeboreshwa. Kamera zote ni 48MP, ina zoom ya hadi 8x, na sasa inakuja na lens mpya ya 200mm, ikiwa ni moja ya simu zenye uwezo mkubwa zaidi wa upigaji picha na video kwa sasa. Uzinduzi huu pia umeleta mshangao kwa wengi baada ya Apple kutambulisha iPhone Air, simu mpya kabisa isiyo na jina la namba tofauti na utaratibu wa kawaida. iPhone Air ni iPhone nyembamba zaidi kuwahi kutengenezwa, lakini yenye uwezo wa kifaa cha kiwango cha juu kama iPhone 17 Pro. Inakuja na kamera ya 48MP, lensi za 26mm hadi 52mm, selfie kamera ya 24MP, uwezo wa kurekodi 4K kwa 60fps, na inatumia chip ya iPhone Pro. Kutokana na muundo wake wa kisasa, classic na wa kuvutia, iPhone Air tayari imeanza kushika kasi mtandaoni, huku watumiaji wengi wakionesha kuvutiwa na muonekano wake wa kipekee pamoja na uwezo wa hali ya juu, licha ya mwonekano wake mwembamba. Apple inaendelea kuonesha kwamba teknolojia ya simu janja bado ina nafasi kubwa ya ubunifu.
Read More