Argentina yatinga fainali ya Kombe la Dunia Qatar 2022

Argentina yatinga fainali ya Kombe la Dunia Qatar 2022

Timu ya taifa ya Argentina imefanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Dunia Qatar 2022 kufuatia kuibutua timu ya taifa ya Croatia bao 3-0 katika mchezo uliochezwa uwanja wa Lusail Jumanne Disemba 13. Julian Alvarez amefunga magoli mawili moja likiwa ni juhudi binafsi ikichagizwa na uzembe wa walinzi wa Croatia na kisha maajabu ya Messi yakapelekea bao la tatu. Sasa Argentina wameingia fainali na watapambana na mshindi kati ya Ufaransa na Morocco ambaye atajulikana siku ya Jumatano. Argentina wamerudia historia ya mwaka 1990 ambapo walifika fainali ya kombe la dunia licha ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Cameroon kwa bao 1-0. Mwaka huu Argentina waliingia katika kombe la dunia na kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Saudia Arabia kwa bao 2-1.

Read More
 Argentina kukutana na Uholanzi robo fainali kombe la Dunia

Argentina kukutana na Uholanzi robo fainali kombe la Dunia

Timu ya Taifa ya Argentina imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la Dunia baada ya kuitandika Australia 2-1 katika mchezo uliokuwa wa kusisimua Nahodha Lionel Messi akiwa kwenye kiwango bora zaidi alipachika bao moja kabla ya Alvarez kutumia vyema makosa ya mlinda lango wa Australia kupachika bao la pili kwa Argentina Sasa Argentina watakutana na Uholanzi katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo na kurudisha kumbukumbu ya mwaka 1998 timu hizo zilipokutana kwenye hatua kama hiyo na Uholanzi kushinda 1-0. Ikumbukwe timu ya Taifa ya Uholanzi iliilaza Marekani 3-1 katika mchezo wa hatua ya 16 bora.

Read More