Ben Pol aomba msamaha EX wake Arnelisa kwa kumzungumzia vibaya

Ben Pol aomba msamaha EX wake Arnelisa kwa kumzungumzia vibaya

Msanii wa Bongo Fleva Ben Pol ameandika barua ya wazi kumuomba msamaha aliyekuwa wake Anerlisa kutoka nchini Kenya kwa kile alichozungumza. Akifanyiwa mahojiano na mtangazaji Millardayo Ben Pol alieleza kuwa hakuwahi kufurahia ndoa yake na Anerlisa. Baada ya mahojiano hayo Anerlisa alimuomba Ben Pol aache kumzungumzia na akaahidi endapo ataendelea basi atapost meseji zake kwani anqchoongea kwenye media ni tofauti na anachomtumia. Sasa  kupitia ukurasa wake wa Instagram ameeleza kuwa lengo lake lilikuwa kueleza namna alivyopitia magumu na kuathirika kisaikolojia hakuwa na lengo na kumuumiza aliyekuwa mke wake Arnelisa. Ben Pol amechukua hatua hiyo mara baada ya Arnelisa kuanika hadharani meseji ambazo msanii huyo alikuwa akimtumia kupitia WhatsApp akitaka warudiane.

Read More
 Arnelisa aanika hadharani meseji za Ben Pol

Arnelisa aanika hadharani meseji za Ben Pol

Mwanadada mjasiriamali kutoka nchini Kenya, Anerlisa ameamua kuweka wazi mapungufu ya Ben Pol, ameachia meseji za msanii huyo wa Bongofleva ambazo alikuwa akimtumia kupitia WhatsApp tangu mwishoni mwa mwaka jana. Jumbe hizo ambazo zimeanikwa hadharani na mtandao wa Mpasho, zinaonesha Ben Pol akimkumbusha Anerlisa matukio ya maisha yao na kumueleza hisia zake, akitaka warudiane. Sakata hili lilianza baada ya Ben Pol kufanya mahojiano na mtangazaji Millard Ayo, ambapo alikaririwa akisema hakuwahi kufurahia ndoa yao na ilikuwa ya mapicha picha tu. Ni madai ambayo yalikanushwa vikali na Anerlisa ambaye alitumia insta story kumuonya Ben Pol asiongelee masuala ya mahusiano yao mitandaoni, vinginevyo atamuanika.

Read More
 Anerlisa ampa onyo Ben Pol ataka aache kumuongelea

Anerlisa ampa onyo Ben Pol ataka aache kumuongelea

Mrembo kutoka Kenya Anerlisa ambaye alikuwa mke wa msanii wa Bongofleva Ben Pol ameonyesha kutofurahishwa na kile ambacho alikizungumza Ben Pol kwenye mahojiano yake na Ayo Tv kuwa hajawahi kufurahishwa na ndoa yake na mrembo huyo. Kupitia InstaStory yake  anashangaa ni kwanini Ben Pol kila siku amekuwa akiongea mambo mengi ili aonekane mbaya mbele ya umma. “Ben naona umenizoea na unachukulia ukimya wangu kama udhaifu wangu. Ulikuwa na uwezo wa kumwambia anaekuhoji asikuulize kuhusu mimi. Kwa nini unapenda kila mara mimi nionekane mbaya. Chini ya kapeti unanitumia jumbe tofauti tofauti na namna unavyoniongelea”, Aliandika. Lakini pia amemtaka Ben Pol aache kumuongelea kwani yeye pia ana mengi kumuhusu lakini amechagua kukaa kimya kama mwanamke. “Kama kweli wewe ni mwanaume, nakuomba uweke wazi jumbe zote ulizokuwa unanitumia tangu Desemba 25 hadi Januari 4, 2023. Nina mengi ya kuzungumza kuhusu wewe au kuonyesha, lakini nimechagua kusimama kama Mwanamke.” , Aliandika.

Read More