Mrembo Arnelisa Muigai akata penzi la mwanamuziki Dufla Diligon

Mrembo Arnelisa Muigai akata penzi la mwanamuziki Dufla Diligon

Huenda juhudi za mwanamuziki Dufla Diligon zikagonga mwamba baada ya mrembo Arnelisa Muigai kukataa hadharani ombi la msanii huyo kutaka kuingia naye kwenye mahusiano ya kimapenzi. Kupitia ukurasa wake wa Instagtam Arnelisa amesikitishwa na kitendo cha Dufla kutumia sarakasi nyingi mtandaoni kwa ajili ya kuteka hisia zake huku akisema kuwa mapenzi hayalazimishwa. Kauli ya Arnelisa imekuja mara baada ya video kusambaa mtandaoni ikiwaonyesha wasanii KRG The Don na Arrow Boy kwenye moja ya night club wakimliwaza Dufla Diligon ambaye alikuwa analilia penzi la Arnelisa. Utakumbuka wiki kadhaa zilizopita Dufla alijitokeza wazi na kudai kuwa anatamani kuingia kwenye mahusiano na Arnelisa ambapo alienda mbali zaidi na kuachia wimbo wake uitwao Arnelisa uliokuwa ukisifia urembo wa Arnelisa. Hayo yamekuja baada ya Arnelisa kutangaza hadharani kukamilisha mchakato mzima wa kuvunja ndoa yake na mwanamuziki bongo fleva Ben Pol.

Read More
 Ben Pol akanusha kukamilika kwa talaka yake na Arnelisa Muiga

Ben Pol akanusha kukamilika kwa talaka yake na Arnelisa Muiga

Mwimbaji wa Bongofleva, Ben Pol amejitokeza na kusema kuwa hajapata taarifa yoyote kuhusu kukamilika kwa talaka na aliyekuwa mke wake, Anerlisa. Wiki iliyopita Anerlisa ambaye ni binti wa seneta wa Nakuru Tabitha Karanja alitangaza kuwa mchakato wa talaka yake na Ben Pol umekamilika. “Mimi pia naona ripoti hizi mtandaoni. Sijafahamishwa rasmi au kwa njia isiyo rasmi. Sijui hayo mawasiliano aliyapata wapi maana hata mahakama niliyofungua kesi ya talaka haifahamu taarifa hizo,” Ben Pol aliambia Nation. Utakumbuka wawili hao walifunga ndoa Mei 2020 katika Kanisa Katoliki la St Gaspar huko Mbezi Beach, Tanzania.

Read More
 Arnelisa yupo uhuru, Akamilisha talaka yake na Mwanamuziki Ben Pol

Arnelisa yupo uhuru, Akamilisha talaka yake na Mwanamuziki Ben Pol

Ni rasmi kuwa mfanyabiashara wa Kenya Anerlisa Muigai na mwanamuziki kutoka Tanzania Ben Pol sio mke na mume tena. Anerlisa ambaye ni binti wa seneta wa Nakuru Tabitha Karanja kupitia ukurasa wake wa Instagram, amefichua kuwa talaka yake na mwimbaji huyo wa Bongofleva hatimaye imekamilika. Mrembo huyo amewashukuru mawakili wake kwa kuhakikisha kuwa mchakato wa talaka yake umekamilika “Niko huru rasmi. Haitakuwa sawa kutowatambua mawakili hawa wawili ambao walifanya kazi bila kuchoka kuhakikisha kwamba talaka inafanywa haraka na sio kusubiri kwa miaka. Hamza Jabir na Hosea Chamba, asanteni kwa kazi zenu na kwa kufanya kila kitu mlivyoombwa.” alisema kwenye Insta stori. Anerlisa na Ben Pol walifunga ndoa Mei mwaka 2020 lakini wakatengana mwaka jana ambapo Ben Pol aliwasilisha kesi ya talaka mahakamani.

Read More
 ARNELISA AFUNGUKA WANAUME KUPENDA PESA ZAKE WANAPOKUWA KWENYE MAHUSIANO NAYE

ARNELISA AFUNGUKA WANAUME KUPENDA PESA ZAKE WANAPOKUWA KWENYE MAHUSIANO NAYE

Mrembo na Mjasiriamali nchini, Anerlisa amesema kuna ex wake alitaka amfungulie biashara jambo ambalo alilikataa na huo ukawa mwisho wa kuachana. Kupitia instastory yake amezungumzia pia suala la kuomba fedha kila wakati katika mahusiano kitu ambacho alikuja kubaini kuwa watu wanaenda kwake kwa ajili kujinufaisha na sio mapenzi. “Nilikuwa kwenye mahusiano ambapo mwenzi wangu alianza kuniambia nimwambie PIN ya ATM, wakati mwingine nikiongea na mama yangu anataka kujihusisha na mazungumzo yetu” amesema “Wacha nicheke mmoja wa ex wangu aliniuliza tumekuwa pamoja kwa mwaka mmoja kwa nini nisimsaidie kama vile kumjengea nyumba na hata kumfungulia kampuni kama yangu, nilimjibu ni kamwambia kama uliona kuanzisha uhusiano na mimi kutakutajirisha haya basi uko kwenye uhusiano ambao haufai,” amesema Anerlisa. Utakumbuka Anerlisa aliwahi kuolewa na Staa wa Bongofleva, Ben Pol lakini ndoa yao ikadumu kwa muda mfupi, katika mapenzi yao mrembo huyo alitokea kwenye video ya wimbo wake Ben Pol, Kidani.

Read More
 ARNELISA MUIGAI KWENYE PENZI JIPYA BAADA YA NDOA YAKE NA BEN POL KUINGIWA NA UKUNGU

ARNELISA MUIGAI KWENYE PENZI JIPYA BAADA YA NDOA YAKE NA BEN POL KUINGIWA NA UKUNGU

Huenda Ex wa msanii wa Bongofleva Ben Pol Arnelisa Muigai yupo kwenye Penzi jipya baada ya kudokeza Kuhusu hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram. CEO huyo wa Life still water na mrithi wa shamba la Keroche Arnelisa Muigai amedokeza hilo kwa kupost kwenye insta story yake emoj ya kopa kama ishara ya mapenzi, ikiwa ni miezi kadhaa tu baada ya kuvunjika kwa ndoa yake/ na kupeana talaka na aliyekua mumewe Ben Pol. Aidha Mkurugenzi Mtendaji huyo aliingia kwenye headlines mapema wiki hii wakati wa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kuonekana na mtu aliefanana na Ben Pol kwenye video ambayo ilisambaa mitandaoni akiwa amekaa kimahaba na mtu huyo ambae hajamuweka wazi kama ndie mpenzi wake wa sasa.

Read More