AROMA AJIUNGA NA LEBO TEAM NO SLEEP

AROMA AJIUNGA NA LEBO TEAM NO SLEEP

Msanii kutoka Uganda Aroma alipata umaarufu kwenye muziki wake kupitia wimbo uitwao Yoola ambao aliwashirikisha wasanii wa B2c Boys. Tangu wakati huo amekuwa akiachia magoma makali ambayo yanazidi kufanya vizuri kwenye chati mbali mbali za muziki. Aroma, ambaye amekuwa akifanya na uongozi wa Butterfly Entertainment inaonekana amefanya mabadiliko kwenye kazi yake ya muziki. Taarifa mpya ni kwamba mrembo huyo amejiunga na lebo ya Team no sleep ambayo inamilikiwa na jeff kiwa na tayari ameachia nyimbo mbili ambazo ni “Omugenyi Omukulu” na “Check Yo Lover”. Aroma anajiunga na wasanii wengine kama Grenade na Pinky ambao tayari wapo chini ya lebo hiyo. Aroma alianza muziki mwaka  2018 alipoachia wimbo wake wa kwanza “Wakimala”  ambao alirekodi na prodyuza Skales huko Kampala lakini akaachia video yake Julai mwaka wa 2019 ambayo ilimtambulisha kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda.

Read More
 AROMA ATISHIA KUWAANIKA HADHARANI WASANII WANAOHUJUMU MUZIKI NCHINI UGANDA

AROMA ATISHIA KUWAANIKA HADHARANI WASANII WANAOHUJUMU MUZIKI NCHINI UGANDA

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Aroma hana furaha kabisa na baadhi ya wasanii  nchini humo ambao wanalipa vyombo vya habari kuhujumu muziki wake. Katika mahojiano na Runinga ya NBS Aroma amesema kuna msanii mmoja wa kike nchini Uganda ambaye anahonga vituo vya redio na runinga sizicheze nyimbo zake. Hitmaker huyo wa “Yoola” amemtaka msanii huyo ambaye anajaribu kuhujumu muziki wake kukoma mara moja na badala yake aelekeze nguvu zake kwenye ishu ya kuwakuza wasanii chipukizi. Hii sio mara ya kwanza kwa wasanii wa uganda kutoa malalamiko juu wasanii ambao wanahujumu kazi za wenzao kupitia vyombo vya habari kwani mwaka wa 2021 tuliona wasanii kama Naira Ali, Bruno K, na Lydia Jazmine wakiwasuta vikali wasanii wanaohonga vituo vya redio na runinga kucheza nyimbo zao huku wasanii wengine wakisahaulika.

Read More
 AROMA ATOA POVU ZITO KWA MASTAA WAKUBWA UGANDA, ADAI WANAUA VIPAJI

AROMA ATOA POVU ZITO KWA MASTAA WAKUBWA UGANDA, ADAI WANAUA VIPAJI

Msanii wa kike kutoka nchini Uganda Aroma amesikitishwa na namna wasanii wakubwa nchini humo wanaendesha tasnia ya muziki. Akiwa kwenye moja ya interview Aroma amedai kwamba mastaa wengi nchini uganda wamehujumu kazi za wasanii chipukizi kwani wamekuwa na mazoea ya kuzihonga vyombo vya habari ili nyimbo zao zichezwe. Hitmaker huyo wa “Yoola” amesema mastaa wengi nchini uganda hawana vipaji kwani wamekuwa wakizitangaza nyimbo ambazo hazina ubora kwa kuwalipa madejaay wa vituo vya redio na runinga. Ikumbukwe pia Juzi kati wasanii kama Naira Ali na Sama Sojah aliwatolea uvivu baadhi ya wasanii wanaolipa vyombo vya habari ili kazi zao zichezwe

Read More