Arrow Bwoy Aitetea Taasisi ya Ndoa
Msanii kutoka Kenya, Arrow Bwoy, ameingilia kati mjadala unaoendelea mitandaoni kuhusu mada ya “Marriage hubamba mafala” iliyoanzishwa na socialite Chebet Ronoh. Chebet alizua gumzo kubwa akidai kwamba ndoa ni ya mafala (wajinga), kauli ambayo imewagawa mashabiki mtandaoni. Wengi wamekuwa wakitoa maoni tofauti, huku baadhi wakiunga mkono na wengine kupinga vikali. Akizungumza kwa mtazamo wake, Arrow Bwoy amesema kuwa yeye binafsi haoni tatizo la ndoa na anajivunia maisha ya kifamilia. Ameongeza kuwa wao kama vijana hawapaswi kubeza ndoa kwa sababu hata wazazi wao waliishi katika ndoa na wakafanikiwa kulea familia zao. Kwa maoni yake, ndoa ni jambo la hiari na lina pande mbili, nzuri na mbaya na kushindwa kwa mtu mmoja hakumaanishi kwamba taasisi ya ndoa haina maana kwa kila mtu. Msanii huyo amesisitiza kuwa kuanzisha mitazamo ya kupinga ndoa kunaweza kuwapotosha vijana, akihimiza kila mtu afanye maamuzi kulingana na maisha yake binafsi.
Read More