ASAP Rocky Azima Tetezi za Albamu ya Pamoja na Young Thug
Rapa maarufu kutoka Marekani, ASAP Rocky, amevunja kimya na kuzima uvumi uliokuwa ukisambaa mitandaoni kuhusu uwezekano wa kutoa albamu ya pamoja na Young Thug. Tetezi hizo zilianza kushika kasi jana baada ya ASAP Illz, mmoja wa wanachama wa ASAP Mob, kuashiria uwezekano wa collabo hiyo kupitia ujumbe wa kuvutia kwenye mitandao ya kijamii. Hata hivyo, ASAP Rocky amekatisha matumaini ya mashabiki kupitia mtandao wa X kwa kuweka wazi kuwa hilo halipo kwenye mipango kwa sasa “FALESE MY BROTHER, UY SCUTI OTW” kwa tafsiri ya haraka: “Umesema uongo kaka, UY Scuti iko njiani”. Aliandika Kauli hiyo inaonyesha kuwa badala ya albamu ya pamoja, ASAP Rocky anajiandaa kuachia mradi wake binafsi unaoitwa UY Scuti, ambao tayari umeanza kuvutia hisia miongoni mwa mashabiki wake. Ingawa collabo kati ya Rocky na Thug bado ni ndoto kwa sasa, mashabiki sasa wanasubiri kwa hamu kufahamu zaidi kuhusu UY Scuti, huku wakifuatilia kila dalili kutoka kwa rapa huyo anayejulikana kwa ubunifu na mitindo isiyotabirika.
Read More