Msanii Marya Alazwa Hospitalini Baada ya Kiharusi, Aomba Msaada wa Kifedha

Msanii Marya Alazwa Hospitalini Baada ya Kiharusi, Aomba Msaada wa Kifedha

Msanii maarufu wa Kenya, Marya, anayekumbukwa kwa kibao chake maarufu Chokoza alichomshirikisha Avril, kwa sasa amelazwa hospitalini baada ya kupata kiharusi (stroke). Taarifa zilizotolewa na marafiki wake wa karibu, akiwemo msanii Avril, zinaeleza kuwa Marya amekuwa akiendelea kupokea matibabu hospitalini kwa muda, na anatarajiwa kuruhusiwa hivi karibuni. Hata hivyo, hali yake bado si nzuri kwani amepooza upande mmoja wa mwili wake, hivyo atahitaji huduma ya karibu ya nyumbani. Katika ujumbe wake, Avril alieleza kuwa Marya anahitaji msaada wa kifedha ili kuandaa mazingira salama na yenye huduma bora nyumbani. Msaada huo unahitajika kwa ununuzi wa vifaa maalum kama kitanda cha hospitali, kiti cha magurudumu, godoro maalum, na vifaa vingine vya matibabu. Avril pia alitoa wito kwa mashabiki na Wakenya kwa ujumla kuendelea kumuombea Marya ili apate nafuu na aweze kurejea katika hali yake ya kawaida. Marya aliwahi kuwa mmoja wa wasanii wakubwa nchini, akijizolea umaarufu kupitia Chokoza na nyimbo nyingine zilizowahi kutamba. Ingawa amekuwa kimya kwa muda mrefu katika tasnia ya muziki, mchango wake bado unakumbukwa na wengi. Kwa sasa, jamii ya wanamuziki, mashabiki na Wakenya kwa jumla wanahimizwa kuungana kwa moyo wa utu na mshikamano, ili kumpa Marya matumaini na msaada anaohitaji katika kipindi hiki kigumu. Kwa yeyote anayetaka kuchangia, mchango unaweza kutumwa kupitia nambari ya simu 0723 207 376 kwa jina la Lilian Miring’u.

Read More
 Avril Afichua Chanzo cha Malipo Duni kwa Wasanii nchini Kenya

Avril Afichua Chanzo cha Malipo Duni kwa Wasanii nchini Kenya

Msanii na mwigizaji wa muda mrefu, Judith Nyambura maarufu kama Avril, ametoa kauli nzito kuhusu malalamiko ya wasanii wa Kenya kuhusu malipo duni kutoka kwa Chama cha Hakimiliki ya Muziki Kenya (MCSK). Akizungumza katika mahojiano ya moja kwa moja na Buzzroom Kenya, Avril alibainisha kuwa mzizi wa tatizo hauko kwa MCSK pekee kama inavyodhaniwa, bali uko kwa taasisi na mashirika yanayocheza muziki wa Kenya bila kulipa ada za leseni. Avril alieleza kuwa malipo ya wanachama wa MCSK yanategemea moja kwa moja kiwango cha fedha kinachokusanywa kutoka kwa wadau kama vituo vya televisheni, redio, vilabu vya burudani na waandaaji wa matamasha. “Sijitetetei wala kuitetea MCSK, lakini tukifanya hesabu, ni vipi taasisi kama MCSK itoe mgao wakati wale wanaopaswa kulipa hakimiliki hawafanyi hivyo?” alisema Avril. Akitumia takwimu kueleza hali halisi, Avril alisema kuwa licha ya ongezeko la wasanii waliosajiliwa, mapato yanayosambazwa yameendelea kuwa haba. Alifichua kuwa mwaka wa 2023, MCSK ilikusanya KSh139.2 milioni pekee. Kwa wanachama 16,000, kila mmoja alipokea wastani wa KSh8,700 kwa mwaka. Aliongeza kuwa hata katika hali ambapo MCSK ingekusanya KSh1 bilioni, malipo kwa kila msanii bado yangekuwa karibu KSh100,000, kiwango ambacho hakitoshi kugharamia hata mradi mmoja wa muziki. Kwa mujibu wa Avril, mzigo mkubwa uko kwenye sera hafifu za ukusanyaji wa ada badala ya mfumo wa usambazaji wa mapato. “Sera za ukusanyaji ndizo zinazofeli mfumo huu, si usambazaji wa mapato,” alisema. Aidha, alisisitiza kuwa wasanii hawawezi kuendelea kutegemea malipo ya hakimiliki pekee kama chanzo cha kipato. “Sekta ya ubunifu inahitaji wawekezaji wakubwa na wadau wapya, kwa sababu wasanii hawawezi kuishi kwa kutegemea royalty peke yake,” alihitimisha. Kauli ya Avril imezua mjadala mpya kuhusu mustakabali wa haki za wasanii nchini, huku wadau wa sekta ya burudani wakihimizwa kuangalia upya sheria na sera ili kuhakikisha wasanii wanalipwa haki zao ipasavyo na tasnia ya muziki inakuwa endelevu.

Read More
 Avril na Tanasha Donna wasikitishwa na kampuni ya ZUKU kukatiza huduma za mtandao bila ilani

Avril na Tanasha Donna wasikitishwa na kampuni ya ZUKU kukatiza huduma za mtandao bila ilani

Wasanii Avril na Tanasha Donna wameonesha ghadhabu zao kwa kampuni ya Zuku kutokana na huduma duni ya mtandao. Kupitia mitandao yao ya kijamii wasanii hao wawili wametoa malalamiko yao kwa kampuni hiyo kufuatia kukosa huduma ya mtandao kwa kipindi cha siku tatu mfululizo. Hata hivyo wameichana kampuni ya Zuku kwa hatua ya kuwa na wahudumu wasiowajibikia majukumu ya kujibu simu za wateja wao wakati wa dharura huku wakitshia kuhamia makampuni mengine ambayo yanatoa huduma ya mtandao.

Read More
 Avril afunguka sababu ya kuitosa Kolabo ya Mr. Seed

Avril afunguka sababu ya kuitosa Kolabo ya Mr. Seed

Mwanamuziki Avril amefunguka madai ya kuitosa kolabo ya msanii mwenzake Mr. Seed mwaka wa 2021. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Avril amesema hakuweza kufanya kazi ya pamoja na msanii huyo kwa sababu kipindi hicho alikuwa ameshikika na masuala ya kuitayarisha album yake ya Spirit. Hitmaker huyo wa “Chokoza” ameahidi kufanikisha kolabo yake na Mr. Seed hivi karibuni pindi tu ratiba zao zitakapokuwa sawa. Kauli yake imekuja mara baada ya mr. Seed kudai kuwa Avril amekuwa akikwepa kufanya nae kazi kwa muda wa miaka minne sasa licha ya kumkumbusha kila mara. Haikushia hapo alienda mbali zaidi na kudai kuwa wimbo wake wa ndoa alipaswa kumshirikisha Avril lakini kilichotokea na kumvunja moyo ni kitendo cha msanii huyo kuanza kumchunia kwa kutojibu meseji zake, hivyo akaamua kurekodi wimbo huo na mwigizaji Kate the Actress.

Read More
 AVRIL AKANA KUWAHI KUTOKA KIMAPENZI NA DIAMOND PLATNUMZ

AVRIL AKANA KUWAHI KUTOKA KIMAPENZI NA DIAMOND PLATNUMZ

Msaniii Avril amekanusha madai kuwa alikuwa na fursa ya kuchumbiana na Diamond Platinumz lakini akachezea nafasi hiyo. Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Avril amesema madai hayo hayana ukweli wowote kwani uhusiano wake na bosi huyo wa WCB ilikuwa ya kikazi na wala sio wa kimapenzi. “Sijawahi kupata nafasi ya kutoka kimapenzi na Diamond Platnumz, lakini ni rafiki mzuri sana kwangu. Amekuwa rafiki yangu kwa muda mrefu sasa lakini hatuzungumzi mara kwa mara. Lakini anapokuwa ananipigia simu au mimi nikimpigia kwa ajili ya kutaka msaada wa jambo fulani, huwa tunaelewana.” alisema Avril. Aidha amepuzilia mbali uvumi unaotembea mtandaoni kuwa amekuwa na mazoea ya kumsikiliza Diamond Platnumz nyimbo zake kabla ya kuingia sokoni kwa kusema kwamba alifanya hivyo mara moja tu na sio vinginevyo. Utakumbukwa mwaka 2012 Avril alitokea kwenye video ya wimbo wa Diamond Platnumz uitwao “Kesho” kama video vixen kitendo kilichowaaminisha walimwengu kwamba huenda mrembo huyo alikuwa kwenye uhusiano ya kimapenzi na msanii huyo wa Bongofleva.

Read More
 AVRIL AFUNGUKA JUU YA UKIMYA WAKE KWENYE MUZIKI

AVRIL AFUNGUKA JUU YA UKIMYA WAKE KWENYE MUZIKI

Staa wa muziki nchini Avril amewajibu wanaodai kuwa hajakuwa akiachia nyimbo kila mara licha ya kuwa na kipaji kikubwa cha muziki. Katika mahojiano na Mungai Eve, Avril amesema kuwa amekuwa akiachia nyimbo kila mwaka ila watu hawajakuwa wakifuatilia kazi zake kama kipindi cha nyuma kwa sababu hapendi suala la kutengeneza matukio kwa ajili ya kuzungumziwa mtandaoni. Aidha amefunguka ya wimbo wake mpya kutopata wafuasi wengi kwenye mtandao wa youtube kwa kusema kwamba alijihisi vibaya wakati watu walianza kumfanyia mzaha mtandaoni huku akidai kuwa ni changamoto ya kazi. Hata hivyo amewataka mashabiki zake kukaa m amedokeza ujio wa ep mpya ya pamoja na prodyuza Saint P ambayo kwa mujibu wake itaingia sokoni hivi karibuni. Avril ambaye yupo chini ya lebo ya muziki ya Digit One Music anafanya vizuri na album yake ya Spirit ambayo ina zaidi ya streams millioni 2 kwenye mtandao wa Boomplay.

Read More