Ngoma Mbili za AY Zachukuliwa Kuzingatiwa kwa Tuzo za Grammy

Ngoma Mbili za AY Zachukuliwa Kuzingatiwa kwa Tuzo za Grammy

Mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, AY, amepiga hatua kubwa katika taaluma yake baada ya nyimbo zake mbili, “Simuoni” aliyomshirikisha Harmonize na “Wanganeka” aliyomshirikisha Kanjiba, kuidhinishwa kuzingatiwa kwa uteuzi wa kuwania Tuzo za Grammy za 68. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, AY amethibitisha taarifa hizo akieleza kuwa hii ni hatua ya kihistoria si kwake tu binafsi, bali pia kwa muziki wa Bongo Fleva na tasnia ya muziki wa Afrika Mashariki kwa ujumla. Nyimbo hizo zimewasilishwa bila msaada wa producers wa kimataifa wala ushirikiano wa wasanii wa nje, jambo ambalo AY amesema ni ushindi mkubwa kwa muziki wa asili ya Tanzania na nchi jirani. Ameeleza pia shukrani zake kwa wadau waliomsaidia katika mchakato wa submissions, akiwemo Tash Stam na Igloo Entertainment, akiwataja kuwa watu muhimu katika safari ya kukuza sekta ya muziki wa Afrika Mashariki kimataifa. AY amesema sasa macho yote yameelekezwa kwenye hatua inayofuata ya uteuzi rasmi wa Grammy nominations, na amewataka mashabiki pamoja na wadau wa muziki kuendelea kumuombea na kumpa sapoti.

Read More