B Classic akiri kutamani penzi la mwanasholaiti maarufu mtandaoni Shakilla

B Classic akiri kutamani penzi la mwanasholaiti maarufu mtandaoni Shakilla

Msanii B Classic ameweka wazi matamanio ya kumchumbia mrembo maarufu mtandaoni nchini Kenya Shakilla kwa kigezo kuwa lazima awe mlokole. Kupitia instastoy yake amesema yuko tayari kuingia kwenye mahusiano na Shakilla huku akidai kuwa atafanya kila awezalo kuhakikisha kuwa mrembo huyo anafurahia maisha yake ya ndoa. “Shakila ! I have seen unataka kutoka soko – Niko soko pia and I can take you in. Na nikupe maisha poa Tu. Ila are you willing to change? I’ll cater for everything. Bora tu nione unakua church girl. Haijalishi it will take how long,” Aliandika Instastory. Kauli ya B Classic imekuja mara baada ya Shakilla kukiri hadharani kuwa hakuna shabiki yake anayetaka kuingia naye kwenye mahusiano ambayo yataishia kuwa ndoa. “So outta all of my followers, no one wants to enter into a serious relationship with me. Was I meant to be in the streets for life?” aliandika Instastory. Ikumbukwe mwezi mmoja uliopita Shakilla alidai kuwa hatokuja kuchumbiana na wanaume wa Kenya ambapo alienda mbali zaidi na kuhoji kuwa heri atoke kimapenzi na wanaume wa Nigeria kutokana na ukarimu wao.

Read More
 B CLASSIC AACHIA KAZI YAKE YA MWISHO

B CLASSIC AACHIA KAZI YAKE YA MWISHO

Msanii wa muziki nchini Kenya, Dennis Manja maarufu kama B Classic ameachia wimbo wake wa mwisho baada ya kutangaza nia yake ya kutaka kuacha muziki.   B Classic alidai kuwa anaacha muziki na kugeukia kazi ya ufundi wa magari baada ya kutoridhishwa na mapokezi ya kazi zake pindi anapoachia muziki mpya.   B Classic mkali wa wimbo wa Pisi Kali uliofanya vizuri mapema mwezi Agosti mwaka huu, ameachia  ‘Utawezana Kweli’, wimbo anaodai kuwa itakuwa kazi yake ya mwisho.   Wimbo huo umetayarishwa na Prodyuza Denzel huku video ikaongozwa na Director Rahim chini ya lebo ya muziki ya Champions Studio yenye makao yake jijini Nairobi.            

Read More