KUNDI LA B2C ENT. LAKANUSHA KUPATA HASARA KWENYE TAMASHA LAO LA MUZIKI
Wasanii wa kundi la B2C kutoka Uganda wamekanusha tetesi zinazotembea mtandaoni kwamba walipata hasara kwenye tamasha lao la muziki lililokamilika juzi kati. Kwenye mahojiano yao hivi karibuni wasanii hao wamesema madai hayo hayana ukweli wowote ikizingatiwa kuwa tamasha lao lilipata mapokezi mazuri kutoka kwa mashabiki na kuingizia faida maradufu. Kauli ya Kundi la B2C Ent imekuja baada ya watu kuhoji kuwa hasara waliyopata kufuata tamasha lao la muziki kutopata mapokezi mazuri ndio sababu iliyopelekea kuchelewesha kwa malipo ya baadhi ya watoa huduma waliofanikisha tamasha hilo. Wamesema ingawa waliingia kwenye ugomvi na baadhi ya watoa huduma waliofanikisha tamasha lao la muziki kuhusu suala la malipo lakini walifanikiwa kukamilisha madeni yao.
Read More