B2C ENT WAAHIRISHA ZIARA YAO YA MUZIKI BARANI ULAYA

B2C ENT WAAHIRISHA ZIARA YAO YA MUZIKI BARANI ULAYA

Wasanii wa Kundi la B2C Entertainment kutoka Uganda wametangaza kusitisha ziara yao ya muziki iliyopaswa kuanza rasmi mwezi huu wa Juni huko barani Ulaya. Kupitia taarifa waliyochapisha kwenye mitandao yao ya kijamii wasanii wa kundi hilo kwa masikitiko makubwa wamesema wamelazimika kupiga chini show hiyo kwa sababu ambazo zipo nje ya uwezo wao. Hata hivyo wamewaomba radhi mashabiki wao wote ambao kwa njia moja au nyingine wameathirika na uamuzi wao huo huku wakiahidi kufanya ziara nyingine kama hiyo barani Ulaya siku za mbeleni. Utakumbuka B2C walipaswa kufanya shows zao nchini Uturuki, Ujerumani na Uingereza Juni 4, 5 na 6 mtawalia.

Read More
 B2C WAWEKA WAZI TAREHE YA KUFANYIKA KWA TAMASHA LAO

B2C WAWEKA WAZI TAREHE YA KUFANYIKA KWA TAMASHA LAO

Kabla ya kuzuka kwa Covid-19, kundi la B2C kutoka uganda lilifanikiwa kuandaa matamasha mawili lakini kwa bahati mbaya walilazimka kusitisha kutokana na makali ya corona. Baada ya kufunguliwa tena kwa uchumi nchini uganda, B2C wiliahidi kuandaa maonyesho mapya. Sasa habari njema ni kwamba wasanii wa b2c wametangaza tarehe ya tamasha lao lijalo. Kupitia mitandao yao ya kijamii, tamasha hilo limepangwa kufanyika tarehe Septemba, 16 mwaka wa 2022. Sehemu ambayo tamasha hilo litafanyika bado haijathibitishwa lakini duru za kuaminika zinasema kuwa tamasha la B2C litafanyika Freedom City. Wasanii wengine wanaotarajiwa kufanya matamasha yao ya muziki mwaka huu ni pamoja na Jose Chameleone, na Pallaso.

Read More