Mbosso Amtaka Diamond Kuvunja Ukimya Kuhusu Kauli za Baba Levo
Mwanamuziki Mbosso ameibuka na kuweka wazi msimamo wake kufuatia mvutano unaoendelea mitandaoni kati yake, Diamond Platnumz, na Baba Levo, kuhusu tuhuma za kushirikiana kumchafua kwa jina au kazi zake. Kupitia mitandao yake ya kijamii, Mbosso amesema kwa uwazi kuwa hana ukaribu wowote na Baba Levo, na hivyo hawezi kushirikiana naye kwa jambo lolote, tofauti na madai yanayoenezwa. Amefafanua kuwa yeye si mtu wa migogoro, na kwamba anamuheshimu Diamond kama kiongozi na kama msanii mkubwa aliyechangia ukuaji wa muziki wake. Hata hivyo, Mbosso amesisitiza kuwa ni wajibu wa Diamond kuzungumza hadharani kumkemea Baba Levo, kwani ukimya wake unaweza kutafsiriwa kama kukubaliana au kuunga mkono vitendo vya matusi na kejeli vinavyotolewa hadharani na Baba Levo. Kauli ya Mbosso imekuja muda mfupi baada ya Baba Levo kumuomba msamaha na Diamond Platinumz akidai kuwa hana ajenda yoyote na Mbosso ya kumchafulia brand yake. “Mzee Lukuga, sina Agenda yoyote na Mbosso na wala siwezi kupanga njama yoyote na Mbosso, nisamehe mzee wangu” Aliandika Instagram. Ikumbukwe jana kulizuka sintofahamu kati ya Mbosso na Baba Levo baada ya Baba Levo kudai kuwa ngoma ya Pawa imetungwa na Diamond Platnumz, ambapo Mbosso alikasirika na kudai huenda WCB inamfanyia figisu wakati aliondoka salama na anaheshimu sana mchango wao kwenye muziki na mara zote amekuwa akiwashukuru.
Read More