Maandy aachia rasmi EP yake mpya Baddies Need Love
Mwanamuziki kutoka nchini Kenya, Maandy ameachia rasmi EP yake mpya iitwayo ‘Baddies Need Love’ EP hiyo yenye jumla ya ngoma tano za moto. ina kolabo tatu kutoka kwa wasanii kama Charisma, Okello Max, Watendawili, na Ywaya Tajiri. ‘Baddies Need Love EP’ ina ngoma kama Ficha, Decide, Si kawaida, Mnoma na Baddies Need Love yenye imebeba jina la EP. EP hiyo ambayo imetayarishwa na maprodyuza kama Metro, Suka Doba na Sirav, inapatikana kwenye majukwaa yote ya muziki (digital platforms). EP mpya ya Maandy inaashiria maendeleo makubwa katika safari yake ya usanii, ikichanganya mitindo mbalimbali ya muziki na sauti bunifu zinazodhihirisha ukuaji wake kama msanii.
Read More