Kenya Kuandaa Mashindano ya Kikapu ya Afrika Kanda ya Tano na Mchujo wa BAL Mwezi Ujao

Kenya Kuandaa Mashindano ya Kikapu ya Afrika Kanda ya Tano na Mchujo wa BAL Mwezi Ujao

Kenya imepata heshima ya kuwa mwenyeji wa mashindano ya kikapu ya Afrika kanda ya tano pamoja na mchujo wa kufuzu kwa ligi ya Basketball Africa League (BAL) kwa wanaume, yatakayofanyika mwezi ujao. Kwa mujibu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Nchini (KBF), mashindano ya wanawake yataanza kuchezwa kuanzia tarehe 9 hadi 15 Novemba katika uwanja wa Nyayo Stadium jijini Nairobi. Michuano hiyo itashirikisha vilabu kutoka Kenya, Rwanda, Tanzania, Burundi na Uganda, huku Kenya ikiwakilishwa na KPA na Zetech University. Baada ya hapo, Kenya pia itakuwa mwenyeji wa mashindano ya mchujo ya BAL yatakayowaleta pamoja mabingwa kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika watakaowania nafasi za kufuzu kwenye ligi ya BAL. Michuano hiyo itafanyika tarehe 18 hadi 23 Novemba katika ukumbi wa michezo wa Kasarani. Nchini Kenya, mashindano hayo yataongozwa na Nairobi City Thunder, mabingwa wa ligi kuu ya taifa, ambao watawakilisha nchi katika kipute hicho. Thunder inalenga kuendeleza mafanikio yake baada ya kufuzu kwa awamu ya timu 12 msimu uliopita bila kupoteza mchezo hata mmoja.

Read More