Usalama wa Eddy Kenzo waimarishwa- Asema Promota Balaam Barugahara

Usalama wa Eddy Kenzo waimarishwa- Asema Promota Balaam Barugahara

Promota Balaam Barugahara amethibitisha kuwa usalama wa mwanamuziki Eddy Kenzo umeimarishwa baada ya kutishiwa maisha na watu wasiojulikana. Kwenye mahojiano yake, promota huyo amesema njama ya wanaopanga kumtoa uhai Kenzo haitafaulu kamwe ikizingatiwa kuwa msanii huyo tayari ana walinzi wengi waliojihami na silaha kali za moto. Baalam ameongeza kuwa njama hiyo inaweza tu kufanikiwa iwapo watesi wake watatumia njia ya uchawi. “Wale wanaotaka kumuua Kenzo wanaweza tu kufanikiwa kupitia uchawi. Ameimarisha usalama wake na walinzi wenye uzoefu,” Balaam alisema kwenye mahojiano na YouTuber mmoja nchini Uganda. Mapema wiki hii, Kenzo alifichua kuwa anapokea jumbe za kumtishia maisha ambapo alienda mbali zaidi na kuwataka Waganda kumuombea.

Read More
 PROMOTA BALAAM BARUGAHARA AAPA KUWAPIGA MARUFUKU WASANII WANAOSUSIA SHOWS UGANDA

PROMOTA BALAAM BARUGAHARA AAPA KUWAPIGA MARUFUKU WASANII WANAOSUSIA SHOWS UGANDA

Promota wa muziki nchini Uganda Balaam Barugahara Atenyi ametishia kuwapiga marufuku wasanii wanaosusia shows licha ya kulipwa pesa zote kwa wakati. Katika mkao na waandishi wa habari Jiji Kampala Balaam Barugahara amesema kamati ya waandaji wa maonesho ambayo inaongozwa na Promota Abtex ina mpango wa kuwapiga wasanii wa sampuli hiyo marufuku ya miaka 2 bila ya kuwapa mialiko kwenye matamasha yeyote ya muziki. Kauli yake imekuja baada onesho lilofanyika huko Kyotera, Mukono nchini Uganda kukumbwa na vurugu ambayo ilisababisha uharibifu mkubwa wa mali ya mamilioni ya pesa. Vurugu kwenye show hiyo ilitokea baada ya jenerata kuzima ghafla kutokana na ukosefu wa mafuta jambo ambalo lilipelekea waliokuwa wamehudhuria onesho hilo kukosa uvumili na kuzua rasbsha kufuatia waandaji wa show kuchukua muda mrefu kuwasha jenerata. Lakini pia msanii Pallaso analaumiwa kwa kuchukua muda mrefu kujitayarisha ndani ya gari lake kabla ya kufika jukwaani kuwapa mashabiki burudani.

Read More