Diana Marua afunguka baada ya kupata ukosoaji mkubwa alipovalia mavazi ya Balenciaga

Diana Marua afunguka baada ya kupata ukosoaji mkubwa alipovalia mavazi ya Balenciaga

Msanii Diana Marua amefunguka kwa mara ya kwanza baaada ya watu kumkosoa mtandaoni kwa kuvalia vazi la Balenciaga licha ya kampuni hiyo kupata ukosoaji mkubwa kutokana na kufanya matangazo ambayo yanakiuka maadili ya watoto. Akizungumza na mume wake Bahati, Diana amesema kuwa hakuwa na ufahamu kuwa chapa ya Balenciaga ilikuwa na utata na ndio maana alivalia vazi lao akiwa tu kwenye shughuli zake za kawaida. Aidha bahati amemtaka awe makini anapochagua mavazi ya kuvaa kwani huenda ikamleta shida mitandaoni ikizingatiwa kuwa kuna baadhi ya makampuni ambayo hufanya matangazo ambayo yanakwenda kinyume na maadili ya jamii. Utakumbuka kampuni ya Balenciaga iliomba msamaha juu ya matangazo yenye baada ya kufanya photoshoot ya bidhaa zao mpya ambayo inadaiwa kuendekeza maudhui ya ponografia kwa watoto.

Read More
 Balenciaga waachana na Kanye West

Balenciaga waachana na Kanye West

Mtandao wa Tmz umeripoti kuwa kampuni ya mitindo na mavazi kutokea Paris, Ufaransa imeamua kuvunja ushirikiano katika uzalishaji wa mavazi kati yao na rapa kutoka nchini Marekani, Kanye West. “Balenciaga haina mpango wa kuendelea na ushirikiano kati yetu na Kanye West”- Chanzo cha kuaminika kutokea Tmz Chanzo hicho hakijaweka wazi sababu ya kampuni hiyo kuachana na rapa huyo wakati wiki kadhaa zilizopita Kanye alikuwa mmoja wa washiriki katika onyesho kubwa la mavazi ya kampuni hiyo huko jijini Paris.

Read More