Barack Obama ataja nyimbo zake pendwa 2022

Barack Obama ataja nyimbo zake pendwa 2022

Rais mstaafu wa 44 wa nchini Marekani, Barack Obama amezitaja nyimbo zake 25 ambazo zimefanya vizuri kwa upande wake kwa mwaka huu Mwaka huu ametaja ngoma 25, katika ngoma hizo ngoma kadhaa za wasanii kutoka Afrika zimetajwa. Mfano “Rush” ya Ayrastarr , “Last Last” ya Burna Boy na “Calm Down” ya Rema. Hii ni dalili tosha kwamba Label ya Mavins Records inafanya kazi nzuri sana kwani Rema na Ayra ni member wa label hiyo. Lakini pia inaonekana Obama ni shabiki mkubwa wa Burna Boy maana hata mwaka 2019 alitaja “Anybody” kama ngoma yake bora. Na wakali wengine walioingia kwenye orodha hiyo ni pamoja na Kendrick Lamar, Beyonce, Lizzo, Bad Bunny na wengine wengi.

Read More