Rapa Barak Jacuzzi Aalikwa Kwenye Pambano la Ndondi

Rapa Barak Jacuzzi Aalikwa Kwenye Pambano la Ndondi

Bondia kutoka Kenya Portifas Odipo, anayefahamika kama Majembe Majembe ameibua mjadala mkali mtandaoni baada kutangaza hadharani anataka kuzichapa na rapa Barak Jacuzzi kupitia pambano la ndondi. Majembe Majembe amesema hataki tena kushinda na Jacuzzi kwa maneno ila anataka waandae pambano la ngumi ili mashabiki wa muziki wa hiphop wapate kufahamu nani ndio mkali kati yao. Kwa kuonesha kujiamini kupita kiasi, Majembe Majembe amejinadi kwa kusema kuwa yuko tayari kwa pambano lolote na kwamba hana wasiwasi hata kidogo kuhusu tukio hilo. Majembe amejipakulia misifa kama bondia mwenye uwezo, nguvu na uthubutu wa kumshinda Barak, akimtahadharisha ajipange kuingia naye ulingo. Endapo Barak ataingia ulingoni, pambano hilo linaweza kuwa tukio la kipekee linalochanganya burudani na michezo, na kuvuta umakini mkubwa kutoka kwa mashabiki kote nchini Kenya.

Read More
 Barak Jacuzzi Amshinda Actually Lumu katika Pambano la Celebrity Fight Night

Barak Jacuzzi Amshinda Actually Lumu katika Pambano la Celebrity Fight Night

Msanii wa muziki wa hip-hop nchini Kenya Barak Jacuzzi ameibuka mshindi dhidi ya Youtuber Actually Lumu katika pambano lililosubiriwa kwa hamu la Celebrity Fight Night Showdown lililofanyika wikiendi hii iliyomalizika jijini Nairobi. Mashabiki walijitokeza kwa wingi kushuhudia pambano hilo lililokuwa na msisimko mkubwa, ambapo Barak Jacuzzi alionyesha umahiri na nguvu za kipekee ulingoni, akimdhibiti mpinzani wake katika raundi za mwanzo kabla ya kushinda kupitia uamuzi wa majaji. Actually Lumu, ambaye amejizolea umaarufu kupitia vipande vya vichekesho mitandaoni, alijaribu kulipa kisasi kwa kutumia mbinu za kujihami, lakini alishindwa kuhimili kasi na uzoefu wa Barak Jacuzzi. Mashabiki waliushangilia ushindi huo huku baadhi wakimtaja Barak kuwa mmoja wa mastaa wa burudani wanaoonyesha kuwa na kipaji cha kipekee si tu katika muziki, bali pia kwenye michezo ya ulingoni.

Read More