Bondia kutoka Kenya Portifas Odipo, anayefahamika kama Majembe Majembe ameibua mjadala mkali mtandaoni baada kutangaza hadharani anataka kuzichapa na rapa Barak Jacuzzi kupitia pambano la ndondi.
Majembe Majembe amesema hataki tena kushinda na Jacuzzi kwa maneno ila anataka waandae pambano la ngumi ili mashabiki wa muziki wa hiphop wapate kufahamu nani ndio mkali kati yao.
Kwa kuonesha kujiamini kupita kiasi, Majembe Majembe amejinadi kwa kusema kuwa yuko tayari kwa pambano lolote na kwamba hana wasiwasi hata kidogo kuhusu tukio hilo.
Majembe amejipakulia misifa kama bondia mwenye uwezo, nguvu na uthubutu wa kumshinda Barak, akimtahadharisha ajipange kuingia naye ulingo.
Endapo Barak ataingia ulingoni, pambano hilo linaweza kuwa tukio la kipekee linalochanganya burudani na michezo, na kuvuta umakini mkubwa kutoka kwa mashabiki kote nchini Kenya.