Barcelona Yawania Saini ya Marcus Rashford kwa Mkataba wa Mkopo

Barcelona Yawania Saini ya Marcus Rashford kwa Mkataba wa Mkopo

Klabu ya Barcelona imewasilisha rasmi ombi kwa klabu ya Manchester United ili kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza, Marcus Rashford, kwa mkataba wa mkopo unaojumuisha kipengele cha kumnunua moja kwa moja mwishoni mwa msimu. Taarifa kutoka vyanzo vya karibu na uongozi wa Barcelona zinaeleza kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo anavutiwa na uwezo wa Marcus Rashford na anaamini atakuwa chachu muhimu katika safu ya ushambuliaji ya timu hiyo inayojengwa upya. Ikumbukwe kuwa Rashford alitumia nusu ya msimu wa 2024/2025 kwa mkopo katika klabu ya Aston Villa, ambako alionyesha mwangaza wa kurejea katika ubora wake wa zamani. Akiwa na Villa, Rashford alicheza jumla ya mechi 17, akifunga mabao 4 na kutoa pasi 6 za mabao (assists), na hivyo kuchangia jumla ya mabao 11. Hata hivyo, bado haijafahamika kama Manchester United wako tayari kumwachilia mchezaji huyo kwa mkopo mwingine, ikizingatiwa kuwa ni zao la akademia ya klabu hiyo na bado ana nafasi ya kurejea kwenye kiwango cha juu akiwa na umri wa miaka 27.

Read More
 BARCELONA KUTOTUMIA CAMP NOU MSIMU WA 2023-24

BARCELONA KUTOTUMIA CAMP NOU MSIMU WA 2023-24

Klabu ya Barcelona imethibitisha kufanyia marekebisho ya uwanja wa Camp Nou na wametangaza kuwa timu hiyo msimu wa 2023-24 itatumia uwanja wa Olympic kwenye eneo la Montjuic ndani ya jiji hilo. Uboreshaji utaanza mwezi Juni, baada ya kumalizaka kwa msimu huu, baada ya bodi kuthibitisha kiasi cha €1.5 billion ili kuweza kufanya maboresho ya uwanja huo maarufu duniani. Inatarajia kuwa maboresho yatachukua miaka minne kwa kazi zote kumalizika, hii inamaanisha kuwa Barcelona watapaswa kuhama kwa msimu ujao na kuhamia kwenye uwanja wa Olympic ambao unatumika na timu ya Espanyol. Klabu ya Barcelona itaweza kuutumia uwanja wa Camp Nuo kwa msimu unaofuata, baada ya msimu 2023-24, huku wakitarajiwa kupunguza idadi ya watazamaji kwa asilimia 50 kwa sababu za ujenzi. “Kitakuwa kiwanja bora duniani, ndani ya jiji bora duniani, ndani ya nchi bora duniani” – ameeleza Joan Laporta, Rais Barcelona akiiambia radio ya huko Catalan, RAC1.

Read More