BARNABA AACHIA RASMI ALBUM YAKE MPYA

BARNABA AACHIA RASMI ALBUM YAKE MPYA

Mwanamuziki Barnaba ameachia rasmi Album yake mpya “Love Sounds Different” yenye Jumla ya mikwaju 18 yenye uzito wa miaka (18) ambayo amekuwepo kwenye huu muziki. Album hiyo imesheheni majina mazito yanayotamba kwenye Muziki wa bongo fleva, Kolabo za nguvu zimesogezwa na Diamond Platnumz, AliKiba, Marioo, Kusah, Dayoo, Jux, Lunya, Mbosso, Saraphina, Khadija Kopa, Lady Jaydee, Jay Melody, Lody Music, Nandy, Rayvanny, Platform na wengine akiwemo pia Khaligraph Jones toka Kenya. Jina la Diamond Platnumz mbali na kutokea kwenye wimbo namba 1 “Hadithi” lakini limetajwa kama Mtayarishaji Mkuu wa Album hiyo (Executive Producer) wakiwemo pia watayarishaji wengine kama Abbah Process, S2Kizzy, Man Walter, Chizan Brain, Mr. Simon, Laizer Classic na wengine

Read More
 BARNABA & ZUCHU WAMJIBU ERICO OMONDI ALIYEDAI BONGOFLEVA IMEULIWA NA AMAPIANO

BARNABA & ZUCHU WAMJIBU ERICO OMONDI ALIYEDAI BONGOFLEVA IMEULIWA NA AMAPIANO

Baada ya msanii wa Comedy nchini Eric Omondi kudai kuwa Amapiano imeuwa muziki wa Bongo Fleva,wasanii wa Tanzania Zuchu na Barnaba Classic wameibuka na kupinga hilo. Wasanii hao wamesema kwamba wanachokifanya kwa sasa ni kutaka kukimbizana na nyakati zilizopo kwani kuwa kwenye kiwanda cha muziki ambacho kina ushindani kunahitaji msaani kuwa na ubunifu Barnaba kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika “Bongo Fleva bado ina nguvu sana kuliko Amapiano. Watu wajue Amapiano sio aina ya muziki bali kwa lugha rahisi ni mixing za Dj’s wa Arika Kusini so haitoweza kuuwa Bongo Fleva” Kwa upande wa Zuchu ameandika kuwa “Bongo Fleva haitotokea kufa wasanii wanabadilika hii inaitwa mabadiliko, kujaribu ladha mpya hakujawahi kuuwa soko la muziki. Acha wasanii wajaribu vitu vipya ndio mabadiliko hayo”

Read More