Barnaba Classic awapa somo wasanii kuhusu nidhamu kwenye kazi zao

Barnaba Classic awapa somo wasanii kuhusu nidhamu kwenye kazi zao

Mwimbaji nyota wa muziki wa Bongofleva, msanii Barnaba Classic amewakumbusha wasanii wenzake kuwa na heshima pamoja na nidhamu kwa watu wengine. Barnaba ametumia insta story yake kuwatahadharisha wakumbuke kuna kesho.. “Ndugu zangu wasanii tujifunze heshima na kuheshimu mipaka yetu ya kazi kwa kila mmoja. Lakini pia tujifunze kuwa na upendo kweli na kutoleta mashauzi Mbuzi ambayo kuna muda baadhi ya mambo hayahitaji mbwembwe nyingi kuliko busara. Tuwe na hekima wakati mwingine. Sio kama wengine hatujui kuongea ila tumelelewa kwenye busara.” ameandika Barnaba Classic. “Nimekuwa kwenye huu muziki yapata miaka 18 sasa lakini sijawahi kumdharau anayekuja leo na aliyeanza kabla yangu. Lakini nadhani kuna jambo kubwa najivunia sana katika maisha yangu ya muziki kuishi bila kuzoea watu hata kama nawajua na kuwachukulia poa. Kwa hiyo ndugu zangu wasanii wenzangu, tuwe na nidhamu na mnapofanya mambo ya kuvunja heshima na mipaka muwe mnakumbuka kuna kesho”. amemalizia Barnaba Classic kwenye mfululizo wa jumbe zake kupitia insta story yake.

Read More
 Barnaba Classic ampa nyota Diamond Platnumz

Barnaba Classic ampa nyota Diamond Platnumz

Mwanamuziki wa Bongofleva Barnaba Classic ameamua kumpa Diamond Platnumz maua yake akiwa hai kwa kushiriki kwa asilimia kubwa sana kwenye kuufanya mwaka 2022 kuwa wenye mafanikio kwake. Kupitia Instastory yake amemshukuru Bosi huyo wa WCB kwa kuandika ,”Asante sana Mungu akubariki, umetenda pakubwa sana. Mungu akupe njia njema wengi tufaidike na uwepo wako. Unaroho ya kipekee sana”. Mwaka 2022 Diamond Platnumz alishiriki kwa asilimia kubwa sana kwenye Album ya Barnaba, “Love Sounds Different” ambayo imempa mafanikio makubwa sana ya kimuziki.

Read More
 BARNABA CLASSIC ATIMIZA NDOTO YA KUFANYA KAZI NA MALKIA WA MIPASHO BI. KHADIJA KOPA

BARNABA CLASSIC ATIMIZA NDOTO YA KUFANYA KAZI NA MALKIA WA MIPASHO BI. KHADIJA KOPA

Mwanamuziki nyota kutoka nchini Tanzania Barnaba Classic ametimiza ndoto nyingine kubwa katika hatua za kukamilisha Album yake ijayo ambayo amewashirikisha wakali kibao. Barnaba kupitia ukurasa wake wa Instagram ameeleza kutimiza ndoto yake ya kufanya kazi na Malkia wa taarab Bi. Khadija Kopa huku akithibitsha kuwa atakuwa miongoni mwa walioshirikishwa kwenye Album yake ijayo. Hata hivyo Barnaba ameongeza kuwa album yake  ijayo itaacha kumbukumbu kwenye muziki wa Tanzania.

Read More
 BARNABA KUMVISHA PETE YA UCHUMBA MPENZI WAKE RAYA

BARNABA KUMVISHA PETE YA UCHUMBA MPENZI WAKE RAYA

Staa wa muziki wa Bongofleva Barnaba Classic yupo mbioni kuufungua ukurasa mwingine wa mapenzi kwa tukio la kumvisha pete ya uchumba mpenzi wake wa siku nyingi bibie Raya The Boss ikiwa ni kiashiria cha kuelekea katika ndoa. Barnaba amebainisha ujio wa jambo hilo la kheri kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kushare picha ya pete mbili na kuwapa nafasi mashabiki wake wamchagulie ipi itafaa kumvisha mpenzi wake huyo. “Ipi itafaa, she says Yes ” – ameandika Barnaba. Uhusiano wa wawili hao ulianza mwaka 2018 baada ya Barnaba kuachana na aliyekuwa mpenzi wake.

Read More