Benzema afunguka kujiondoa Ochungulo Family

Benzema afunguka kujiondoa Ochungulo Family

Msanii Benzema amejibu tetesi za kujiondoa kwenye kundi la Ochungulo Family baada  ya kuonekana akifanya kazi zake binafsi. Kwenye mahojiano na SPM Buzz Amesema yeye bado ni mwanafamilia wa Ochungulo ikizingatiwa kuwa kuna kazi nyingi ambayo wamefanya kwa pamoja kama kundi. Aidha amekanusha kuwa kwenye ugomvi na wasanii wanaounda kundi hilo kwa kusema kuwa wana uhusiano mzuri wa ufanyaji kazi huku akiahidi mashabiki watarajie makubwa kwenye muziki wao mwaka 2023. Utakumbuka Agosti 30 mwaka huu kundi la Ochungulo Family ambalo linaundwa na wasanii Nelly The Goon, Benzema na Dmore walitabariki na album iitwayo “Tamasha” ambayo ina jumla ya mikwaju 8 ya moto.

Read More
 BENZEMA AFUNGUKA KUHUSU UTATA UNAOZINGIRA WIMBO WA FOTO MOTO

BENZEMA AFUNGUKA KUHUSU UTATA UNAOZINGIRA WIMBO WA FOTO MOTO

Msanii wa kundi la Ochungulo Family Benzema amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya Noti Flow kudai kuwa hajawahi faidi na mirabaha ya wimbo wao wa “Foto Moto. Katika mahojiano na Mungai Eve, Benzema amesema kipindi walimaliza kurekodi wimbo huo Noti Flow alimuambia kwamba ana haja na wimbo wa Foto Moto kwa kuwa muziki wa Kenya haulipi, jambo lilimfanya achukue wimbo huo na kuuweka kwenye mitandao ya kupakua na kusikiliza muziki. Benzema amesema kwa sasa anaendelea kuingiza kipato kupitia mirabaha ya wimbo wa Foto Moto,  hivyo Noti Flow ndio wakulaumiwa kwa kuwa alikata tamaa mapema juu ya wimbo huo. Utakumbuka wimbo wa Foto Moto wake Noti Flow akiwa amemshirikisha Benzema ilitoka mwaka wa 2020 na video yake kwenye mtandao wa youtube ina zaidi ya views millioni 4.5.

Read More