BEST NASO AACHIA RASMI EXTENDED PLAYLIST (EP) YAKE MPYA

BEST NASO AACHIA RASMI EXTENDED PLAYLIST (EP) YAKE MPYA

Msanii wa Bongofleva, Best Naso ameachia Extended Playlist (EP) mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake. EP hiyo inakwenda kwa jina la Shujaa ina jumla ya nyimbo 11 za moto ikiwa na kolabo 8 kutoka kwa wakali kama Tunda Man, Dully Sykes, Nay wa Mitego, Stamina,Saida Karoli, Young Killer, Country Boy na Kala Jeremiah. Shujaa ambayo kwa sasa inapatikana kwenye majukwaa yote ya ku-stream muziki duniani  ina ngoma kama Number One,Beautiful, Kuoa, Bahati, Hero na nyingine nyingi. Utakumbuka mwaka jana Best Naso aliachia albamu yake ya tatu, The Gift of Life yenye nyimbo 32. Best Naso ameshaachia albamu kama Mamu wa Dar (2009) na Narudi Kijijini (2013), na zote zilifanya vizuri hasa ngoma zilizobeba majina ya albamu hizo.

Read More
 BEST NASO MBIONI KUACHIA EP MPYA

BEST NASO MBIONI KUACHIA EP MPYA

Msanii wa Bongofleva Best Naso ameanika hadharani tracklist ya EP yake mpya inayokwenda kwa jina la Sauti ya Hisia. Kupitia Instagram yake Hitmaker huyo wa ngoma ya “Tamba” amesema EP hiyo ambayo ina jumla ya ngoma 11 ya moto itaingia sokoni rasmi Mei 15 mwaka 2022. Best Naso amewashirikisha wakali kama Dully Sykes, Nay wa Mitego na Stamina huku EP yenyewe ikiwa na nyimbo kama Napendwa, Bahati, Tubadilike, Ajigambe, Single, Happy na nyingine nyingi. Hii project ya kwanza kwa mtu mzima Best Naso kwa mwaka huu ikizingatiwa kuwa amekuwa akiachia ngoma mfululizo bila kupoa katika siku za hivi karibuni. Utakumbuka mwaka wa 2021 mkali huyo wa muziki wa Bongofleva alitubariki na album iitwayo Gift of Life iliyokuwa na jumla ya mikwaju 32 ya moto.

Read More