Wezi Wapora Hard Drives Zenye Kazi Muhimu za Beyonce Jijini Atlanta
Kabla ya maonyesho ya msanii nyota duniani Beyonce yaliyofanyika jijini Atlanta, ripoti zinasema kuwa wezi walivunja magari ya baadhi ya watu wa karibu na msanii huyo na kuiba vifaa muhimu vya kazi. Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na timu ya Beyonce, tukio hilo lilitokea Julai 8 ambapo gari la choreographer na dancer mmoja lilivunjwa na hard drives kadhaa kuibwa. Inadaiwa kuwa vifaa hivyo vilikuwa na kazi ambazo bado hazijatolewa kwa umma, zikiwemo nyimbo mpya, video, mipango ya maonesho ya siku zijazo na nyaraka zingine za kipekee. Hadi sasa, hakuna taarifa rasmi ya kupatikana kwa hard drives hizo, lakini uchunguzi wa kina umeanzishwa na mamlaka za usalama wa mji wa Atlanta ili kuwabaini wahusika na kurejesha mali iliyoibiwa. Tukio hili limeibua wasiwasi miongoni mwa mashabiki kuhusu usalama wa kazi za wasanii na athari zinazoweza kutokea endapo maudhui hayo yatavujishwa mitandaoni bila idhini.
Read More