BIEN WA SAUTI SOL ATAKA WIZARA YA UTAMADUNI KUBUNIWA NCHINI KENYA
Msanii wa Sauti Sol, Bien amependekeza kubuniwa kwa wizara ya masuala ya utamaduni kwa kile alichokitaja kuwa ni nyanja iliyotengwa kwa muda mrefu nchini. Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram Bien amesema hatua ya Kenya kuunganisha michezo na utamaduni huku ikizidi kuipa kipau mbele sekta ya michezo haina mashiko kwa kuwa ni nyanja mbili tofauti ambazo zinapaswa kupewa uzito kwa usawa. Hitmaker huyo wa “Inauma” ametaka serikali kuweka nguvu zaidi kwenye masuala ya utamaduni kama inavyofanya kwa sekta ya michezo kwani mataifa yote yanayoendelea duniani yana wizara ya utamaduni. Kauli ya Bien imekuja mara baada ya Rais wa Kenya William Ruto kutaja baraza lake la mawaziri
Read More