BIEN WA SAUTI SOL ATAKA SERIKALI KUPUNGUZA BEI YA UNGA

BIEN WA SAUTI SOL ATAKA SERIKALI KUPUNGUZA BEI YA UNGA

Msanii anayeunda kundi la Sauti Sol, Bien Baraza amezua gumzo mtandaoni mara baada ya kusema kwamba hatawahi kuwa na amani hadi pale bei ya unga itakaposhuka. Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram Bien amedai kwamba moja kati ya bidhaa ambayo anatamani ishuke bei ni unga wa sima huku akipendekeza iuzwe shillingi 99 za Kenya “You won’t see me smiling till the price of unga goes down to Ksh. 99 #Inauma”, Aliandika Hata hivyo wafuasi wake wameonekana kumfanyia mzaha kwenye uwanja wa comment ya posti yake kwa kusema kwamba itabidi azoee huku wengine wakihoji kuwa anashinikiza bei ya unga wa sima ishuke kwa kuwa anatokea katika jamii ya Waluhya ambayo imekuwa ikihusishwa sana na uraibu wa ugali.

Read More
 BIEN WA SAUTI SOL AWAHIMIZA WAZAZI KUWAFUNZA WATOTO WAO LUGHA YA MAMA

BIEN WA SAUTI SOL AWAHIMIZA WAZAZI KUWAFUNZA WATOTO WAO LUGHA YA MAMA

Mwiimbaji wa Sauti Sol Bien Aime Baraza amefunguka na kudai kuwa atawafunza watoto wake lugha ya kiluhya ambayo ndio chimbuko lake. Katika mahojiano na mpasho Msanii huyo amewahimiza wazazi kuwafunza watoto wao lugha yao ya mama kama njia moja ya kudumisha utamaduni, mila na desturi za kiafrika. Hitmaker huyo wa ngoma ya Mbwe mbwe ameeleza kuwa ana mpango wa kuachia kitabu chake cha hadhithi kiitwacho Bald Man Comic ambacho ni mahusisi kwa ajili ya kusherekea na kutambua mchango wa utamaduni wa kiafrika kupitia fasihi andishi. Huu ni muendelezo mzuri kwa wasanii wa sauti sol ambao katika siku za hivi karibuni wamegeuza muziki wao kuwa biashara ambapo wamewekeza kwenye nyanja mbali mbali  kama njia ya kujiongezea kipato.

Read More