BIEN NA AARON RIMBUI WAACHIA RASMI “BALD MEN LOVE BETTER” EP
Hatimaye msanii wa Sauti sol Bien na Aaron Rimbui wameachia rasmi EP yao mpya inayokwenda kwa jina la “Bald Men Love Better”. Ep hiyo ina jumla ya mikwaju nne ya moto ambazo wamezifanya bila kumshirikisha msanii yeyote. Baldmen love Better EP ina nyimbo kama Mbwe Mbwe, Stamina, Reset Rewind na Baldmen Love Better ambapo inapatikana exclusive kupitia digital platforms mbalimbali za kupakua na kusikiliza muziki duniani. Ikumbukwe uzinduzi wa Baldmen Love Better EP kutoka kwa mtu mzima Bien na Aaron Rimbui utafanyika Novemba 6 mwaka huu jijini Nairobi.
Read More