Big Sean apata mtoto wa kiume

Big Sean apata mtoto wa kiume

Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Big Sean pamoja na mpenzi wake Jhene Aiko wamebarikiwa kupata mtoto wao wa kwanza wa kiume. Big Sean amethibitisha taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kusema kuwa mtoto huyo anaitwa “Noah”. “After 24 hours of Labor, A Lunar Eclipse, with rain from the beginning of labor til he was born, he’s here safe and sound. Happy, Healthy and everything we could ever ask for and more. Any and everything for you Son. Noah 11/8/22,” Aliandika. Jhene na Big Sean wamekuwa pamoja kwa muda mrefu na mtoto huyo atakuwa kifungua mimba kwa ‘couple’ hiyo pendwa.

Read More
 KANYE WEST NA BIG SEAN WAZIKA TOFAUTI ZAO BAADA YA KUWA KWENYE BIFU KWA MUDA

KANYE WEST NA BIG SEAN WAZIKA TOFAUTI ZAO BAADA YA KUWA KWENYE BIFU KWA MUDA

Rapa Kanye West na Big Sean wamemaliza tofauti zao, wameonekana wakiingia studio pamoja. Kwenye picha zinazotembea kwenye mitadao ya kijamii wameonekana pia French Montana, Pusha T, Pressa, Fivio Foreign and The Game. Tetesi zinadai kwamba Kanye west yupo kwenye maandalizi ya album yake ijayo ‘Donda 2’ na huwenda sauti za wakali hao zikasikika kwenye album hiyo. Big Sean na Kanye west waliingia kwenye vita ya maneno mwishoni mwa mwaka jana, hii ni baada ya Kanye west kusema kuwa miongoni mwa vitu ambavyo anajutia kwenye maisha yake ni kumsaini Big Sean. Baada ya kuruka interview hiyo ambayo Kanye west alifanya kwenye Podcast ya ‘Drink Champs’ Big Sean aliomba kukaa kwenye kiti hicho pia na kumjibu Kanye west kwa kusema yote aliyozungumza ni upuuzi mtupu japo heshima yake kwake haiwezi kupotea. Big Sean ambaye aliondoka GOOD Music na kuanzisha label yake,  anamdai Kanye zaidi ya shilling million 147 za Kenya.

Read More
 BIG SEAN AMJIBU KANYE WEST,ADAI ALICHOKISEMA KWENYE MAHOJIANO NA DRINKS CHAMPS NI UJINGA

BIG SEAN AMJIBU KANYE WEST,ADAI ALICHOKISEMA KWENYE MAHOJIANO NA DRINKS CHAMPS NI UJINGA

Rapa kutoka nchini marekani Big Sean amesema anampenda sana Kanye West na anampa heshima zote kwa upendo aliomuonesha kumshika mkono hadi kufahamika, lakini kwa alichokisema kwenye mahojiano na Drink Champs mwezi Novemba mwaka huu ni ujinga mtupu. Big Sean amekuwa mgeni mpya wa Drink Champs, kipindi ambacho kitaruka Jumamosi hii, Sean amesikika akisema “Nampenda Kanye. Nampenda kwa nafasi aliyonipatia na kila kitu. Lakini nafikiri alichokisema kilikuwa ni upuuzi na ujinga mtupu.” amesema Big Sean. Kanye West aliingia kwenye headlines baada ya kusema kwamba miongoni mwa vitu ambavyo anajutia kwenye maisha yake ni kumsaini rapa Big Sean kwenye label yake, GOOD Music.

Read More