STREAMS ZA BOOMPLAY KUHESABIKA BILLBOARD

STREAMS ZA BOOMPLAY KUHESABIKA BILLBOARD

App namba moja ya kupakua na kusikiliza muziki Afrika,Boomplay imefanikiwa kuingiza kazi za wasanii katika chati za Billboard kama sehemu yake ya kuendelea kusaidia tasnia ya muziki wa Afrika kutanua wigo wake kamili. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa umma na Kampuni ya Transsnet Music Limited ambayo ndiyo inayomiliki Programu tumuishi (App) ya Boomplay,  itaanza kuingiza kazi za wasanii katika chati maarufu za Billboard Hot 100, Billboard 200, Artist 100 na Billboard Global 200, na pia chati zingine zote za Billboard Marekani na kimataifa ambazo zinajumuisha kazi za kupakua na kusikiliza muziki. Aidha, pamoja na mamilioni ya nyimbo za Kiafrika kusikilizwa kupitia programu hiyo duniani kote, kujumuishwa kwa taarifa za Boomplay katika chati hizo kubwa za muziki kunawapa wasanii wa Kiafrika na Kimataifa fursa ya kuonekana zaidi kwenye majukwaa makubwa duniani. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ndani ya jukwaa la Music Connect la MRC Data, kazi za Boomplay zitajumuishwa kwenye kapu moja la takwimu linalojumuisha mahitaji ya sauti na picha ambapo picha zimeanza kuonekana kuanzia Oktoba 12, 2021 na miito Oktoba 8, 2021. Streams za Boomplay ziliizoingizwa kwenye chati za Billboard zinawakilisha streams kutoka kwa wasikilizaji waliojisaliji kawaida na wale wa kulipia huku kila stream kutoka kwa msikilizaji wa kundi husika vikipimwa kwa uzito wake.

Read More