Nicki Minaj Aonyesha Upendo kwa Wasanii Chipukizi

Nicki Minaj Aonyesha Upendo kwa Wasanii Chipukizi

Malkia wa muziki wa Rap kutoka Marekani Nicki Minaj ameonyesha upendo kwa kizazi kipya cha wasanii katika mahojiano mapya na Vogue Italia. Rapa huyo mwenye mafanikio makubwa alimtaja Sabrina Carpenter kama msanii anayemvutia kwa ubunifu na mvuto wa kipekee, akieleza kuwa aligundua kipaji chake hivi karibuni licha ya Carpenter kuwa kwenye muziki kwa muda. “Sabrina Carpenter… ni kama pumzi safi ya hewa,” alisema Minaj. “Sikujua kwamba alikuwa kwenye game kwa muda mrefu kiasi hicho nilipoanza kumsikiliza.” Aidha, alimsifu Billie Eilish kwa ubunifu wake wa kipekee katika muziki wa kisasa. Licha ya kutotajwa rasmi, Eilish anasikika katika utangulizi wa albamu ya Nicki Pink Friday 2, ishara kwamba uhusiano wa kisanii kati yao tayari umeanza kuchipua. “Napenda kila kitu anachofanya. Ni msanii wa kipekee sana.”, Nicki alisema. Nicki pia alimpongeza Skeng, msanii wa dancehall kutoka Jamaica, kama mmoja wa wanaoleta ladha tofauti kwenye muziki wa sasa. Akizungumzia mitandao ya kijamii, Nicki alieleza kuwa ingawa ina athari kubwa katika kujenga majina ya wasanii, bado kipaji halisi hujitokeza hata bila ushawishi wa mtandao. “Superstar ni superstar, iwe na mitandao ya kijamii au bila.”, Alilisitiza Minaj. Mashabiki sasa wana matumaini ya kuona mashirikiano ya wazi kati ya Nicki na wasanii hao aliowataja hasa Carpenter, ambaye bado hawajafanya kazi pamoja.

Read More
 Billie Eilish, Eminem, na Beyoncé Wang’ara Tuzo za American Music Awards 2025

Billie Eilish, Eminem, na Beyoncé Wang’ara Tuzo za American Music Awards 2025

Tuzo za American Music Awards (AMAs) 2025 zimefanyika rasmi mjini Las Vegas usiku wa kuamkia Mei 26, zikishuhudia wasanii wakubwa wakituzwa kwa mafanikio yao ya mwaka. Billie Eilish ndiye aliyeibuka kidedea kwa kushinda tuzo saba, ikiwemo Msanii Bora wa Mwaka, Albamu Bora (Hit Me Hard and Soft), na Wimbo Bora (“Birds of a Feather”). Miongoni mwa washindi wengine ni Bruno Mars aliyechukua tuzo ya Msanii Bora wa Kiume wa Pop, Beyoncé aliyeshinda kupitia kipengele cha Country, na Eminem aliyeshinda Albamu Bora ya Hip-Hop kupitia kazi yake The Death of Slim Shady. SZA, The Weeknd, Kendrick Lamar, Bad Bunny, na Lady Gaga pia walitambuliwa kwa mchango wao mkubwa katika muziki. Msanii wa Afrika Kusini Tyla alishinda tuzo ya Msanii Bora wa Afrobeats, huku RM wa BTS akichukua tuzo ya Msanii Bora wa K-Pop. Janet Jackson alitunukiwa Tuzo ya ICON kwa mchango wake mkubwa katika muziki, naye Rod Stewart alipokea Tuzo ya Mafanikio ya Maisha. Hafla hiyo ya kifahari ilijumuisha maonyesho ya kuvutia kutoka kwa wasanii mbalimbali kama Gwen Stefani, Gloria Estefan, na Lainey Wilson, na ilitangazwa moja kwa moja kupitia televisheni ya CBS na huduma ya Paramount+. Mashabiki walifurahia usiku wa muziki uliosheheni burudani na heshima kwa vipaji vikubwa duniani

Read More
 BILLIE EILISH AJUTA KUTIZAMA VIDEO ZA NGONO AKIWA MDOGO

BILLIE EILISH AJUTA KUTIZAMA VIDEO ZA NGONO AKIWA MDOGO

Mwanamuziki kutoka nchini Marekani, Billie Eilish amesema kutazama video za ngono mtandaoni kuliharibu ubongo wake kwani alianza kuzitazama akiwa mdogo. Billie ambaye kwa sasa ana miaka 19 amesema hay wakati akihojiwa kwenye The Howard Stern Show. “Kama mwanamke, nadhani video za ngono ni aibu,” alisema kwenye mahojiano hayo. “Nilikuwa naziangalia sana, kusema ukweli. Nilianza kuangalia pindi nina miaka 11.” Aliendelea,” Nadhani ziliharibu kabisa ubongo wangu na najihisi kuvunjika kabisa kuwa niliangalia sana.” Hitmaker huyo “Lovely” amekiri kuwa ilifika wakati alikuwa akiangalia video zenye vitendo vya kutisha na kikatili zaidi. “Nilikuwa bikira. Nilikuwa sijafanya chochote. Na pia ilinipelekea kwenye matatizo.Mara ya kwanza nafanya mapenzi nilikuwa sikatai vitu ambavyo havikuwa vizuri. Kwasababu nilidhani hivyo ndivyo nilipaswa kuvutiwa navyo,” alisisitiza. “Nina hasira sana kuwa video hizo zinapendwa. Na nina hasira kwangu mwenyewe kwa kudhani ilikuwa sawa.” Muimbaji huyo amekiri kuwa zilimfanya kuwa na fikira zenye kasoro kuhusu tendo la ndoa na mahusiano.

Read More