LIL DUVAL APINGA BLAC CHYNA KUINGIZA KSHS. BILLIONI 2.4 KUPITIA ONLYFANS
Mchekeshaji na Muigizaji Lil Duval ameibuka na kuzungumzia ishu ya Blac Chyna kutengeneza zaidi ya KSh. Bilioni 2.4 kila mwezi mwaka 2021 kwenye mtandao wa OnlyFans. Kupitia mfululizo wa post zake kwenye mitandao ya kijamii, Mchekeshaji huyo amesema huu ni uzushi mtupu na hakuna ukweli wowote. “Siamini kama nyie wote mnaamini Blac Chyna alitengeneza kiasi hicho cha pesa ($20 million) kwa mwezi kupitia OnlyFans. Hapa ndio nafahamu sasa ninyi nyote hamuishi kwenye uhalisia.” aliandika Lil Duval na kucheka kisha kuongeza “Mnaamini kila mnachokiona kwenye vichwa vya habari, na hata hamuulizi. Nimeona Wanawake waki-post na kusema ‘Naweza kuamini’ hii ni ushahidi kwamba nyie wote hamjui ($20 Million) ilivyo. Mmiliki wa OnlyFans ameanika hilo ili kuwapumbaza vichwa vyenu na mfungue akaunti zenu. Namba hazidanganyi, lakini kwa hili wametupanga.” alimalizia Lil Duval.
Read More